Uraibu na Urafiki

Jinsi ya kusaidia rafiki anayehitaji usaidizi.

Aliomba pesa lakini hakutaka kusema alichokusudia kufanyia pesa hizo.

Ukiwa umemjua mtu kwa muda, ni rahisi kumwambia wakati kuna tatizo.

Hii hapa ni hadithi: Tupata ajali ya baiskeli. Nilikuwa salama, lakini alivunjika mkono wake. Daktari alimpa tembe ili kutuliza maumivu. Sasa yuko sawa, lakini aliniambia kuwa hakuacha kumeza tembe. Asingeacha, alisema. Nilishtuka na sikujua cha kusema.

Wakati mtu ana uraibu, hufanya kila kitu anachoweza ili kutatua tatizo. Hafikirii ikiwa vitendo vyake vitamdhuru yeye wala watu wengine. Kama kudanganya, kuiba au kuomba pesa anapojua kuwa hawezi kuzilipa.

Ni vipi mtu anapokuwa mraibu? Kidogo kidogo, hadi akue mtegemezi wa dawa yoyote ya kulevya anayotumia. Rafiki yako anaweza kufikiria au kuwa na tabia tofauti sasa, sio namna alivyokuwa, na hata anaweza kujitenga na kukuepuka.

Kama mgonjwa, watu wenye uraibu wa dawa za kulevya wanahitaji uelewa, usaidizi na upendo.

Nilizungumza na rafiki yangu. Nilimwambia kuwa nisingeweza kumkopesha pesa zozote ikiwa angezitumia kwa kitu kibaya. Lakini nilikuwepo kumjali ikiwa alimhitaji mtu wa kuzungumza naye. Alikasirika sana, akanifokea na kuenda nje.

Nilikuwa na miaka kumi na sita hili lilipotendeka. Aliniomba kuandamana naye hadi kwa daktari, na tangu siku hiyo, ameweza kukabili uraibu wake. Ulihitaji uvumilivu mwingi na mapenzi kutoka kwa familia na marafiki zake kumsaidia.

Kama tu huyu rafiki yangu, ikiwa unamjua mtu yeyote anayepambana na dawa za kulevya, mtafute mtu mzee anayeaminika, kama mwalimu au mzazi, mwombe usaidizi kuhusu tatizo hili.

Mtu anapokuwa mraibu, haipaswi kuwekwa siri. Wakati mwingine, ni vigumu kufanya kitu kinachofaa, lakini ikiwa tunawajali marafiki zetu kabisa, tutafanya chochote tunachoweza ili kuwasaidia.

Share your feedback