Siku mpya iko hapa!

Ota ndoto kubwa. Mustakabali ni wetu!

Hamjambo Wanaspringster!

Jina langu ni Chikondi na nimetoka Zambia. Mwezi uliopita shuleni, mwalimu wetu wa kuigiza alitusimulia hadithi ya ajabu kuhusu mwanamke anayeitwa Oprah Winfrey. Alilelewa na mama mmoja kule Mississippi, Marekani. Utotoni mwake,aliweza kuishi maisha magumu ya umaskini na ubaguzi wa rangi. Lakini hakuruhusu mambo haya kusitisha kutimiza ndoto zake. Alipanda ngazi katika TV na Filamu na kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kupokea tuzo la kipekee Hollywood. Hiyo inatia moyo sana!

Baada ya kusikia hadithi hii nilitafuta kwenye YouTube “speech Oprah Winfrey made” baada ya kushinda tuzo hilo. Ilikuwa nzuri sana. Jambo alilosema na lililonipendeza sana ni:

"Nimewahoji watu walioponea baadhi ya mambo mabaya zaidi katika maisha yao, lakini jambo moja kuu ambalo wote walishiriki pamoja ni uwezo wa kudumisha matumaini ya siku nyingine nzuri, hata wakati wa siku zetu zenye giza zaidi. Kwa hivyo ninawataka wasichana hapa, sasa, kujua kwamba siku nyingine inawadia !"

Wasichana, Oprah Winfrey ako sahihi kabisa! Siku nyingine imekaribia kwa ajili yetu. Sasa hivi, sisi wasichana duniani kote tuna nguvu zaidi ya wakati wowote ule, tuna uwezo zaidi wa kupata maelezo na tumeshirikiana zaidi kuliko awali. Sasa ni wakati wa kujiamini hasa katika ndoto zetu kwa sababu MUSTAKABALI NI WETU! Usiwahi kuamini kwamba wewe ni mdogo sana au haufai kuwezesha ndoto zako zitimie .

Hotuba ya Oprah Winfrey kwa hakika hunifanya niamke na nikifirie kuhusu jinsi pia mimi nilivyo na nguvu ya kufanya ndoto zangu zitimie. Niliongea na wasichana wengine katika darasa langu na kwa pamoja tulipata wazo la kuendesha klabu ya uigizaji , baada ya kuhitimu shuleni ,kwa wasichana katika jamii yetu. Kwa njia hiyo wasichana ambao hawakuenda shule wangewezakujiunga pia. Wiki iliyopita tulionyesha mchezo wetu wa kwanza wa kuigiza kuhusu Malkia Amina wa Afrika.

Ninamshukuru Oprah Winfrey kwa msukumo wake, lakini pia najivunia sana kwa kuchukua hatua ya kuwasaidia wasichana katika jamii yangu. Kama naweza kufanya, pia nawe unaweza, unachopaswa kufanya ni:

  1. Kujiamini
  2. Kuchukua hatua na kufanya mambo yatimie.
  3. Usiwahi kufa moyo hata wakati mambo ni magumu.

Share your feedback