Furaha kwa sekunde 60

Mbinu 3 zenye burudani za kubadilisha uso uliokunjwa :( kugeuza juu chini :)

Hisia zetu zinaweza kuwa kama hali ya hewa. Wakati mwingine tunahisi hatuna furaha kama siku za mvua na dhoruba. Wakati mwingine tuna furaha na ujasiri kama siku yenye joto na jua!

Kurudi kuwa na furaha baada ya kukasirika au kuwa mpweke si rahisi, lakini, INAWEZEKANA.

Hapa kuna mbinu 3 zenye kuburudisha za kubadilisha hii :( kuwa Dansi

Kidokezo 1 - Rocket Ship

Hesabu ukienda nyuma toka 5 hadi 1 na ujifanye wewe ni roketi inayong’oa nanga kwenda hewani. Hivi: 5... 4... 3... 2... 1... NYANYUKA!

Unaposema “nyanyuka”, inuka na uruke juu na uende ufanye jambo linalokupa raha. Songa na uondoe hisia za kuchusha ulizonazo. Kucheza muziki na kudensi ni chanzo bora. Kidokezo hiki ni bora kama unahitaji motisha wa kufanya jambo muhimu.

Kidokezo 2 - Kuandika na Kurarua

Kama wewe hupendi kucheza densi basi jaribu mbinu hii. Inaitwa ‘Kuandika na Kurarua’. Tafuta karatasi na uandike mambo yote mabaya unayohisi. Labda mtu alikukasirisha na una hasira au wivu. Sio vyema kufungia mambo haya. Andika yote kwenye karatasi halafu IRARUE. Ni hisia nzuri kwa sababu ni kama hisia hizo mbaya hazina nguvu kwako tena.

Kidokezo 3 - Kioo, Kioo Ukutani

Kuna uwezo mkubwa kwenye maneno yetu. Je wajua fikra zako huelekeza hisia zako na hisia zako huelekeza matendo unayofanya? Ndio maana ni muhimu kuwa na fikra nzuri na uzizungumze kwa sauti.

Kwa hivyo unapoamka kila siku, jiangalie kwenye kioo na urudie maneno haya:

Najipenda
Nina nguvu
Nimetosha
Ninapendwa
Nina thamani
Mimi ni mrembo
Mimi ni mwerevu
Kuna kusudi maishani mwangu
Ninaweza kutimiza ndoto zangu

Kumbuka, hakuna aliye na furaha wakati wote. Kuwa na huzuni ni kawaida. Unapohisi huzuni ni vyema kukubali hisia zako kisha ujaribu kidokezo kimoja kati ya hivi kuziondoa hisia hizo. Usijifanye kwamba huna tatizo au ukwamilie hisia zako. Zisalimie kisha ziambie kwaheri!

Share your feedback