Imarisha kujiamini kwako: Sehemu ya 2

Ogopa na uendelee

Kuwa mjasiri hakumaanishi kwamba hutaogopa. Inahusu kuogopa kabisa na kuendelea hata hivyo.

Vitu ambavyo hujafanya ndivyo vitu ambayo unaweza kuvibadilisha.

Wakati mwingine sisi huwa macho, tukiwa na wasiwasi kuhusu mambo tuliyoyafanya - au ambayo hatukuyafanya. Ijapokuwa hatuwezi kubadilisha yale tuliyoyafanya, tunaweza kwa hakika kubadilisha yale ambayo hatujayafanya!

Ni kawaida SANA kufikiria na kufikiria kuhusu jambo ambalo unaamini unaweza kulifanya (au kulifanya vizuri sana). Kufikiria kupita kiasi kunaweza kuwa kama kupuliza na kupuliza kiputo, na kutazama wasiwasi ukiendelea kukua. Lakini wakati tunapojaribu, na kuweza kufanya mambo ambayo tunaogopa kuyafanya, ni kama kupasua kiputo cha wasiwasi.

Mara kwa mara, tukujisukuma kulifanya, tutapata hatuwezi kukumbuka ni kwanini tulikuwa na wasiwasi sana kulihusu hapo awali. Na hiyo ndio hisia bora. Kila wakati tunapojisukuma na kushinda uoga na kufikia upande ule mwingine huongezea kujiamini. Tunavyoendelea kuifanya zaidi ndivyo tunavyoendelea kuwa na nguvu zaidi - kana kwamba tunaendelea kuwa wazuri zaidi.

Kwa nini sio sasa?

Fikiria kuhusu jambo ambalo umelitaka kufanya kwa muda sasa lakini hujalifanya.

Si kwamba unapaswa kulifanya sasa, lakini unaweza. Kwa nini basi hujalifanya?

Lifikirie kwa njia hii na mwishowe itahisi ni kama una udhibiti zaidi wa kazi hiyo, badala ya kazi hiyo kukudhibiti. Ni lengo lango - unalimiliki.

Je, itahisi vizuri kuanza tu? Linaonekana ni kubwa sana, unaweza kuligawanya?

Ikiwa kuna kitu unachotaka kuanza kukizungumzia, anza kwa kutabasamu na kusema hujambo. Ikiwa kuna kitu unachotaka kuandika au kuchora, anza na mstari wa kwanza. Kama unataka kukimbia, anza kwa kutembea. Anza tu Kwa sababu unaweza. Na wakati unapofanya, utaweza kujiamini zaidi kwa hatua ifuatayo, na itakayofuata...

Ukiitekeleza, jivunie.

Tunapojilinganisha, inaweza kuonekana kama watu wengine hawafanyi bidii sana. Inaweza kuonekana kama ni rahisi kwao kufanya mambo wanayotaka kuyafanya. Lakini hatujui ni mara ngapi wamejaribu na kushindwa, au kutamani wangeifanya vitofauti. Hatuwezi kujua kwa kweli jitihada ambazo watu wamezifanya kwa tukio hilo moja tunaloliona.

Lakini unajua kazi ambayo umeifanya. Inaweza kuchukua mazoezi kadhaa, lakini inahisi vizuri kusheherekea kwamba, bila kupuuza mafanikio, tunaweza zote kuchukua muda kidogo kufurahia kujivunia tulichotimiza.

Share your feedback