Je, marafiki zako ni wabaya kwako?

Angalia ishara hizi.

Kuna aina nyingi za watu katika ulimwengu huu, na sio kila mtu atakuwa mzuri kwako. Njia bora ya kupata marafiki watakaokufanya kuwa mtu bora zaidi ni kujifunza jinsi ya kuwatambua wale watakaokuangusha.

Rafiki mbaya atakuchochea kufanya mambo ambayo hufurahishwi nayo.
Kwa hivyo ikiwa hufurahishwi kuwa karibu na mtu fulani, au na kitu ambacho anakuambia ufanye, ni wakati wa kukataa.

Wanakukejeli au imani zako.
Rafiki mzuri atakuheshimu na kile unachokiamini. Ikiwa mtu anakuhukumu, kukudhihaki au kukucheka kwa sababu ya dini, sura au uamuzi wako wa maisha – mtu huyo hafai maishani mwako.

Hasikilizi unachokitaka.
Wanyanyasaji au wadhalimu hukutarajia kuwasilikiza bila kuuliza swali. Huenda vikawa vigumu kuwakabili, haswa ikiwa wewe ni mwoga. Lakini ikiwa wanajiona kuwa rafiki zako wanapaswa kujaribu kukujumuisha na kusikiliza maoni yako.

Huhisi vizuri kujihusu ukiwa karibu nao.
Marafiki wazuri wanafurahia ukiwa na furaha. Tahadhari watu ambao hawafurahii, wana chuki au wanazungumza mabaya kuhusu wengine – watajaribu kukufanya hivyo pia.

Kumkataa rafiki mbaya kunaweza kuwa kugumu, lakini kunafaa. Ikiwa unataka kufaulu maishani, tangamana na watu wenye nia safi ambao wataunga mkono ndoto na malengo yako.

Share your feedback