Sababu 5 kuonyesha wewe ni wa kushangaza!

Fikia ndoto zako kwa kuwa na mtazamo unaofaa!

Kuna wakati unahisi ni kama huwezi kufikia ndoto zako?

Niko hapa kukujulisha kitu – unaweza kufikia ndoto zako. Kujiamini ni hatua ya kwanza katika safari ya kufikia ndoto zako.

Kujiamini ni muhimu sana. Hutusaidia kuwa na mtazamo unaofaa na kushinda kila siku. Ujasiri hutusukuma kusonga mbele wakati tunapitia hali ngumu, hata wakati tunahisi kukata tamaa. Tunapokosa ujasiri mambo huonekana magumu kufikia, na hutufanya tujihisi kupungukiwa kukosa motisha.

Kuna mambo mengi unaweza kufanya kujenga ujasiri wako… kwa mfano, kusoma makala haya ya kusisimua ya Springster. Lakini njia bora ya kujenga ujasiri wako ni wewe kujiamini mwenyewe!

Hio ni kweli kabisa! Unashangaza jinsi ulivyo sasa.

Hizi hapa sababu tano:

  1. Wewe ni mfanikiwa! Kutaka kujenga ujasiri wako tayari kunaonyesha kuwa wewe ni mfanya maamuzi mwenye malengo na oliyekusudia.
  2. Una uwezo! Unaweza kushindwa kubeba ndovu kwa mkono mmoja lakini umeweza kukabiliana na hali au kazi ngumu.
  3. Wewe ni mjanja! Kumbuka wakati oliweza kufanya jambo peke yako! Lazima uwe mwerevu sana kufanya ivo.
  4. Wewe ni mkarimu! Una mawazo na nia njema juu ya watu wengine.
  5. Wewe ni jasiri! Hofu au wasiwasi hutokana na msukumo wa kutaka kufanya vizuri katika kitu folani, na si mbaya. Kujiamini haimanishi huna wasiwasi tena, inamaanisha kwamba unaweza kufanya jambo hadi kufikia lengo lako ndani ya hofu yako.

Usidharau tabia zako za sasa ulizonazo. Kujitizama ndani ni njia nzuri ya kugundua ukweli juu ya sehemu zako za kushangaza ambazo tayari unazo.

Hapa kuna zoezi: Andika angalau mambo 3 unayopenda kuhusu tabia yako; labda ni mwenye ndoto kubwa, unachekesha wengine au wewe ni mkarimu.

Kisha, kila wiki, andika jambo moja zaidi. Ukiweza, endelea kuongezea orodha na kuipitia unapojihisi mnyonge.

Kamwe usiache kukubali uzuri wako wa ndani dada!

Share your feedback