Kazi inayokufaa ni gani?

Kazi bora kwako ni ile inayokufaa sifa zako! Fanya jaribio hili la kufurahisha ili kufahamu kazi ambazo zitakufaa.

1. Unapotazama kipindi cha televisheni au filamu, ni nini unachokitambua sana?
A) Asili ya kupendeza na mihemko ya waigizaji
B) Vita, magari yanayofukuzana na athari maalum za kuvutia
C) Gharama ya kutengeneza na pesa ambazo waigizaji walilipwa

2. Unapopanga kuenda kutembea na marafiki au tukio shuleni, ni kauli ipi inayokuelezea vizuri?
A) Ni mimi ndimi ninayewajibikia mambo ya kufurahisha – muziki, michezo na vyakula
B) Ni mimi ndimi ninayehakikisha kuwa kila mtu amealikwa na kuwasili kwa wakati
C) Ni mimi ndimi ninayefanya utafiti wote, kutafuta eneo na kufahamu gharama ya kila kitu
3. Ni aina gani za vitabu unafurahia kusoma?
A) Ubunifu na mapenzi
B) Sayansi, anga, usafiri na ugunduaji
C) Hadithi za kusisimua zilizoshuhudiwa na watu halisi

4. Unapokabiliwa na changamoto ni ujuzi gani unaotumia kuikabili?
A) Nitajaribu kujiondoa katika hali
B) Ninapenda kutumia mikono yangu kwa hivyo nitajaribu kujenga au kuunda kitu kinachoweza kutatua tatizo langu
C) Ninapenda kutafiti au kusoma vitabu shuleni ili kupata majibu

5. Ungalikuwa na mmea au ungalikuwa ukipanda mboga na ukatambua zilionekana kuwa na ugonjwa, ungefanya nini?
A) Ningalizungumza na mimea na kuiimbia
B) Ningalifanya jaribio ili kujitengenezea tiba au kutumia tiba ya asili
C) Ningalifanya utafiti na kuchanganua dalili kisha kujaribu suluhisho bora
Ulipata nini?

A Nyingi
Wewe ni nafsi nyeti yenye ujuzi mwingi wa sanaa. Nguvu yako ni kwamba wewe ni mwenye ndoto na unapenda kuwasaidia wengine. Watu wabunifu hufanya vyema kwenye kazi zinazohusu muziki, uandishi, uanahabari, ufundishaji, mtindo na kazi za jamii.

B Nyingi
Unapenda kufanya majaribio na unataka kuelewa mchakato wa mambo. Kazi ya sayansi, kiwandani, udaktari, kilimo, umekanika au hata tasnia ya vyakula itakufanya kuwa bora.

C Nyingi
Wewe ni mtu ambaye unapenda kufahamu njia sahihi ya kufanya mambo ukitumia utafiti. Ikiwa wewe ni bora kwa hisabati, basi uhasibu au biashara inaweza kukufaa. Ikiwa unapenda kusoma vitabuutapenda kazi ya sheria, serikali au chuoni.

Share your feedback