Nguvu Zako za Kipekee

Unajua kuwa ulikuwa uwezo huu wote ndani yako?

Nguvu Zako za Kipekee

Habari MwanaSpringster!

Tunataka kukueleza siri kubwa. Uko tayari? Sawa, ndiyo hii.

Maisha si rahisi, tuamini, tunaelewa jinsi unavyohisi. Kila wiki huleta changamoto mpya na katika hali ya changamoto hizi sisi sote tuna chaguzi mbili. Kukata tamaa, au kupata nguvu ya kuendelea.

Je, ni chaguo gani unafikiri MwanaSpringster anastahili kuchagua? CHAGUO LA 2, bila shaka! MwanaSpringster anaweza kuhisi kukata tamaa, lakini kisha anakumbuka kuhusu nguvu za kipekee zilizo ndani yake.

Unaweza kuwa unawaza, "Mimi? Nguvu za kipekee? Haiwezekani, mimi ni msichana wa kawaida tu." Wewe si wa kawaida. Ikiwa unasoma hadithi za Springster mara kwa mara na kujiita MwanaSpringster basi una uwezo fulani ambao utakupa nguvu ya kushinda changamoto nyingi.

Nguvu za kipekee za 1: Una UJASIRI

Kuwa MwanaSpringster inakupa sababu 101 za kujiamini. Unapojiamini, inakupa ujasiri unaohitaji kushinda na vikwazo na kubadilisha jamii yako. Kamwe usisahau kuwa wewe ni wa thamani na maisha yako yana sababu. Unaweza kufungulia ujasiri wako kwa kuviamini vipaji na talanta ndani yako, kutia bidii ili kuzikuza, na kisha kuzitumia ili kuwasaidia wengine.

Nguvu za kipekee za 2: Una UWEZO

Ikiwa unahisi kama jambo fulani haliwezekani, kumbuka mambo yote ya kushangaza ambayo wasichana kama wewe wanafanikiwa kuyafikia kila siku kote ulimwenguni! Ikiwa wanaweza kufanya hivyo, unaweza pia. Hivyo unapokumbana na changamoto kubwa, usisahau kamwe uwezo ulio ndani yako ambao unatokana na kuwa msichana.

Nguvu za kipekee za 3: HAUKO PEKE YAKO

Wakati wa hali ngumu, unaweza kupata msaada kutoka kwa marafiki, familia na WanaSpringsters wenzako – hustahili kupitia maisha peke yako. Tuko hapa kwa ajili yako! Ikiwa itafika wakati uhisi kama unalemewa na changamoto, kuomba usaidizi ndilo jambo bora la kufanya!

Kumbuka kujiunga na jamii yetu ya Facebook ili kupata vidokezo zaidi vya Springster