Kuwa mshindi siku nzima, kila siku!

Mambo 7 madogo na muhimu unayoweza kufanya kila siku ili kuishi maisha mazuri

Kuwa mshindi siku nzima, kila siku!

Hujambo Springster!

Je, unajua kwamba unachokifanya kila siku ni muhimu zaidi kuliko unachokifanya mara moja kwa wakati? Hasa wakati wa kujishughulikia mwenyewe. Tabia ni mambo unayoyafanya mara kwa mara. Wakati mwingine bila kugundua kwamba unayafanya. Ni kama ubongo wako hukuambia moja kwa moja cha kufanya.

Tabia zina nguvu kwa sababu zinaweza kukusaidia kuwa bora zaidi au zinaweza kukurudisha nyuma na kukuzuia. Hii ni kwa sababu unachokifanya kila siku, hubadilika kuwa kila wiki kisha kila mwezi na mwishowe kila mwaka. Kwa hivyo ili kushinda katika mwaka, lazima uanze kwa kuwa mjasiri na kushinda siku yako!

Mambo unayoyafanya kila siku yanaweza kukusaidia kuongezea imani yako na kukufanya uhisi vizuri kujihusu. Hapa kuna mambo machache lakini muhimu unayoweza kuanza kufanya ili uimarike!

1. Akili yako nzuri sana

  • Jiambie mambo mazuri kujihusu unapojiangalia kwenye kioo kama vile “mimi ni mrembo” , “nina nguvu” , “ninajipenda!”
  • Usijihukumu wakati mambo yanapoenda vibaya. Wajibika kwa hatua zako na ujifunze kutokana na makosa yako. Kila mtu hukosea kwa hivyo usijilaumu.
  • Chukua hatua kuwazia ndoto zako. Hatua ndogo husababisha mafanikio makubwa, kwa hivyo fanya kitu kidogo kila siku ambacho kinakufanya ukaribie ndoto zako. Kama kuweka akiba ya pesa kidogo kila siku ili uweze kusoma kozi fulani, au kusoma makala kwenye Springster kuhusu jinsi ya kufanya unachopenda katika biashara.

2. Mwili wako mzuri

  • Kula vizuri ni tabia nzuri na hukufanya uhisi vizuri kila wakati! Kunywa maji mengi kila siku na upunguze kula vitu vitamu.
  • Kufanya mazoezi mara kwa mara ni tabia nyingine nzuri ambayo huleta maajabu. Huongezea nguvu yako siku nzima na hukusaidia ujihisi uko na ujasiri zaidi!

3. Marafiki na familia yako nzuri

  • Kuwa mzuri kwa kila mtu karibu na wewe. Kumpa mtu tabasamu kunaweza kusaidia sana kuboresha siku yake. Kutabasamu hukufanya pia uhisi vizuri. Jaribu sasa :) unaona - inafanya kazi!
  • Shiriki ufahamu na wasichana wengine ili nyote mkue pamoja. Kama vile wakati unaposoma makala kwenye Springster, shiriki ulichokisoma na msichana mwingine ili aweze kuwa bora pia! Jiulize," Ni kitu gani kipya nilichojifunza leo?" Kisha mtafute mtu wa kushiriki naye!

Kumbuka hakuna mtu mkamilifu kwa hivyo si rahisi kufanya hivi kila siku. Jambo muhimu ni kuanza na usife moyo!