Mbona kupiga hatua wa kwanza ni sawa!

Nani anasema kuwa ni lazima iwe mvulana atafanya hivi?

Mbona kupiga hatua wa kwanza ni sawa!

Moyo unapiga kwa kasi, unatokwa jasho katika viganja, unasahau cha kusema - mambo haya hukufanyikia? Kuwa na mtu unayemtamani inaweza kuwa hali ya kusisimua sana!

Lakini unafanya nini wanapokosa kuchukua hatua inayofaa na kukualika mtembee nje nao?

Badala ya kusubiri ili mvulana apige hatua ya kwanza - wasichana hawa walichukua hatua ya kwanza na kuwaalika watu waliotamani kwenda nje nao.

Hii ndio sababu kualika mtu unayemtamani kwenda nje na wewe ni sawa!

1. Ujasiri ni mzuri!

Lucie alijua kuwa anampenda Les kutoka wakati alipomwona darasani. Marafiki zake walimwambia kwamba anapaswa kumsubiri amwalike waende nje, huenda akahisi aibu. Lakini Lucie alichoka kusubiri, hivyo akamtumia ujumbe siku moja kumuuliza kama angependa kutembea kutafuta chakula pamoja.

Les akamjibu mara moja. Lucie anafuraha sana kuwa alipiga hatua ya kwanza na kila wakati Les humwambia kuwa ujasiri wake na kujua anachotaka ndicho kinachomvutia kwake.

2. Huenda asiwe na ujasiri wa kukualika

Wavulana wanaweza kuwa na haya na uoga wa kualika watu wanaotamani kwenda nao nje. Kwa kushiriki hisia zako, mtu unayemtamani anaweza kuhisi utulivu zaidi na kuondokewa na hofu.

Kwa hivyo ikiwa unachumbiana na mtu na wewe ni mwenye urafiki, kupiga hatua ya kwanza ndilo jambo la busara zaidi.

Asha alikuwa amemtamani Imran kutoka kwaya kwa miezi mingi. Lakini kila wakati alipomkaribia, Imran alijawa na haya na kuondoka.

Asha alichukua udhibiti na kumwachia kidokezo kwenye mfuko wake ili kumualika waende nje kununua aiskrimu baada ya kipindi cha kwaya wiki inayofuata.

Imran alijawa na furaha sana na akamwambia kwamba alifurahia wakati Asha alipomwalika kwa sababu alikuwa akitaka kufanya hivyo kwa miezi kadhaa lakini hakuwa na ujasiri.

3. Maisha yako ya mapenzi yanakuhusu WEWE!

Ni rahisi kuwa na wasiwasi kuhusu kile ambacho watu watafikiri au jinsi mvulana atahisi - lakini unapaswa kuwa mkweli kwa hisia zako. Hatua ya kujenga maisha ya mapenzi unayotaka huanza na wewe!

Emi alikuwa ameanza kuwa na hisia kwa Nash, rafiki wa ndugu yake. Hisia hazikuondoka, hivyo akamwalika wawe na matembezi ya kirafiki.

Baada ya kukutana mara kadhaa, Emi aligundua kuwa hakuwa na hisia za kimapenzi. Emi ana furaha sana kuwa alipiga hatua wa kwanza, hivyo alipata uhakika na kugundua mambo mapya tena.

Mambo yanaweza kosa kwenda jinsi yalivyopangiwa. Mtu unayemtamani huenda asishiriki nawe hisia zake za kimapenzi - na hilo ni sawa! Watu wengi watahisi tu kupendezwa, lakini ikiwa wanasema kitu chochote hasi, basi hawakuwa bora kwako. Unapaswa kujivunia kwamba ulikuwa mwaminifu na hisia zako na hupaswi kuomba msamaha kwa hilo.