Mwongozo rahisi kwa urafiki wa kimapenzi

Kuwa na furaha na kamili

Mwongozo rahisi kwa urafiki wa kimapenzi

Unafikiria kuhusu urafiki wa kimapenzi? Hauko pekee yako! Urafiki wa kimapenzi ni sehemu ya kawaida ya kukua. Na inaweza kuwa yenye furaha!

Kwa hiyo, ni bora kuwa katika uhusiano salama na mzuri. Ambao una furaha, kamili na starehe. Ambao kwa hakika unaweza kuwa mwenyewe. Vidokezo hivi vitakusaidia kuanza:

Kuwa marafiki

Uhusiano bora huanza na urafiki. Uhusiano bora hujengwa na uaminifu, usawa na kuheshimiana. Unapoanza kama marafiki, mambo haya yatakuja kwa urahisi.

Ni muhimu kujuana kwanza kabla ya kuwa na hisia kubwa. Utaweza kuona kama mnapenda mambo sawa, mawazo, thamani, n.k. Utaweza pia kuona kama huyu ni mtu anayekuheshimu na kukushukuru wewe ulivyo.

Zungumza

Unapokuwa na mtu, unapaswa kuwa huru kuzungumza nao. Kama kuna jambo linalokusumbua, ni bora kulizungumzia badala ya kuliweka ndani. Kwa mfano kama mpenzi wako anakuhimiza kufanya mapenzi na hauko tayari, unapaswa kuzungumza kuhusu maoni yako na hisia. Mpenzi wako hawezi kusoma akili yako. Kuwa wazi, moja kwa moja na mkweli iwezekanavyo.

Usiwe siri ya mtu yeyote

Jambo bora zaidi kuhusu kuwa katika uhusiano? Kukutana na wapendwa wa kila mmoja! Kama huwezi kumwambia rafiki wako wa dhati kwamba unauhusiano na mtu, kuna tatizo fulani. Vilevile kama mpenzi wako anataka kukutana na wewe tu maeneo ya siri ambapo hamtaonekana pamoja, unafaa kuuliza swali. Ni mapenzi kweli kama wanaogopa kuonekana na wewe hadharani? Fikiria kuhusu hilo.

Unapaswa iwezekane kukaa na marafiki wa kila mmoja. Itawasaidia kujua kila mtu alipo.

Tenga muda wako binafsi

Kuwa katika uhusiano haimaniishi lazima muwe pamoja kila wakati. Mnahitaji muda wenu binafsi. Haufai kuwawacha marafiki zako kwa sababu una urafiki wa kimapenzi. Au uwache kufanya mambo uliyopenda. Mara kwa mara, pumzika na fanya mambo yako. Kuna furaha kuwa pekee yako pia.

Kuwa mkarimu na mwenye msaada

Hakuna kuitana majina ya kuvunjiana heshima au kunyamaziana. Hakuna kupigiana kelele au kupigana - haijalishi jinsi ulivyokasirika. Daima inuana juu, badala ya kuwekana chini. Amini ndoto za kila mmoja na shangilia kila mmoja. Ndiyo, mtatofautiana wakati mwingine. Lakini mambo yanaweza kusuluhishwa na mbinu sawa na ya kiutu mzima.

Kumbuka, unastahili kuhisi salama, mwenye kupendwa na kukubaliwa. Una haki ya kuondoka kwa uhusiano unaohisi huna furaha na sio salama. Kama una tatizo kuhusu uhusiano wako, zungumza na mtu mzima unayeamini mara moja.