Uchanganuzi wa Kikosi

Tunaweza kuwa tofauti lakini sisi sote tunapenda kuwa marafiki pamoja

Uchanganuzi wa Kikosi

Umewahi kutofautisha jinsi ulivyo kati yako na marafiki zako? Wanaweza kukufanya ujihisi mwendawazimumu na wakati mwingine kuna drama na kutoelewana. Lakini ukifikiria, tofauti hizi katika kila mmoja katika kikosi chetu ndizo huongezea uzuri, furaha, na urembo katika maisha yetu.

Katika ucheshi na drama katika muda wako pamoja, ni tabia gani zinazoibuka katika kundi lako? Tumejumlisha tabia nyingi katika kundi la marafiki, je, wewe ni yupi?

Dada Mkubwa

Yeye ndiye mama kati yenu. Hulea. Hujali. Huwa na karatasi ya shashi kwa wanaolia na vitafunio kwa wenye njaa. Yeye hukufunza kuzingatia mahitaji ya wengine.

Meya

Anajua kila mtu na huongea na kila mtu. Anaweza kuongeleshwa kwa aina yoyote ya msaada au ushauri. Hukutia msukumo kuhusu jinsi ya kumfanya mgeni kuwa rafiki.

Mgumu

Mlinzi wa kikosi chako. Si mwoga na ako tayari kumtetea kila mtu katika kundi. Hukufanya uone kwamba chini ya ugumu wake kuna moyo mwepesi na unaowalinda wale anaowapenda.

Mfanya biashara

Ana fikra kuhusu pesa na biashara. Ana tamaa ya makuu. Anajua jinsi ya kutafuta njia za kupata pesa wakati hakuna yeyote kati yenu ana pesa. Hukufunza kuokoa na kukuza pesa zako.

Mtaalamu wa Urembo

Huyu ni mrembo na mwenye roho nzuri. Anaweza kutegemea kwa vidokezo vya kujipodoa na fesheni. Atakusaidia kuona urembo wako mwenyewe na kukufunza jinsi ya kuuboresha.

Mcheshi

Yeye ndiye anayeonekana sana na kila mtu anayetaka kusikiliza hadithi zake. Huchangamsha kila mtu mwenye huzuni. Mjanja lakini anapendeza. Hukuonyesha kwamba nyakati mbaya hazitakuwa mbaya sana ukiwa kati ya watu wanaofaa.

Kila mtu katika kikosi chako ana uwezo na ujuzi wake mwenyewe. Kwa hivyo furahieni tofauti zenu! Kuna thamani ya ajabu hata katika nyakati za kila siku katika urafiki wenu. Utajifunza kuwa na watu tofauti na wewe, na kuingiwa na huruma, kuongeza uwezo wako wa kupenda, na kupanua akili yako.