Kupekua Matokeo Hayo ya Utafutaji

Ni kubofya kupi ambako ni hatari na ni kupi kwa kweli? Tunayo majibu!

Kupekua Matokeo Hayo ya Utafutaji

Wasichana wa Springster wanajua kuwa mtandao unaweza kuwa mahali pa ajabu. Unaweza kujiburudisha wewe mwenyewe kwa michezo, vitabu, muziki, na filamu. Unaweza kujiunganisha na watu ulimwenguni kote. Unaweza kujifunza kuhusu chochote unachotaka kwa utafiti rahisi. Ajabu!

Kwa bahati mbaya, sio kila kitu ambacho kiko kwenye mtandao ni kizuri — au sahihi — hivyo wasichana wa werevu lazima wajue kutambua habari bandia.

Kwa kila kitu kinachoendelea ulimwenguni sasa hivi, unaweza kujikuta unatafuta kwenye mtandao ili kujaribu kupata habari zaidi kuhusu vitu kama vile virusi, chanjo, na majanga.

Huenda ikawa tayari una baadhi ya ujuzi wa kutambua udanganyifu, lakini huu ni wakati mzuri wa kujikumbusha wewe (na marafiki na familia yako!) jinsi ya kupata vyanzo vya kuaminika vya taarifa na habari. Hizi hapa ni njia chache tunazozipenda zaidi:

Taarifa ziko kwenye Taarifa

Unapotafuta taarifa … mahali pema pa kuanzia ni ‘taarifa’! Magazeti na taarifa za utangazaji (yaani taarifa zilizo kwenye runinga) mara kwa mara huwa vyanzo vya kuaminika vya habari.

Gazeti kuu na kituo cha runinga katika nchi yako au mji huenda ikawa chanzo cha kuaminika na sahihi, lakini ni muhimu kukumbuka kuwa baadhi ya vyombo vya habari hulenga zaidi burudani kuliko ukweli, hivyo unaweza kumuuliza mtu mzima wa kuaminika, kama vile mwalimu au mzazi, mapendekezo iwapo huna uhakika ni chombo kipi cha habari kilicho chaguo bora.

Unaweza pia kuangalia ukweli wewe mwenyewe kupitia Mtandao wa Uchunguzi wa Ukweli wa Kimataifa (ICFN) kwenye WhatsApp. Ukibofya kiungo hicho, utapata orodha ya nchi na nambari za WA za matawi tofauti ya ICFN. Kutuma ujumbe kwa ICFN kwenye WA ni bure, na ni njia nzuri!

Oh, na usisahau: vituo vingii vya runinga na magazeti huwa na tovuti na wasifu wa mitandao ya kijamii, hivyo unaweza kufikia habari zote kwenye mtandao bila kuhitaji runinga au kulazimika kununua gazeti.

Tovuti Rasmi ya COVID-19 ya Serikali ya Kenya

Ulimwenguni kote, serikali nyingi za maeneo husika zimeunda tovuti maalum za COVID-19, na Serikali ya Kenya haijaachwa kwa hili! tovuti ya Wizara ya Afya_ imejaa habari kutoka kwa madaktari na wanasayansi wetu walio bora nchini. Ina vidokezo kuhusu jinsi ya kukaa ukiwa mwenye afya na maelezo yote kuhusu jinsi ya kupata usaidizi wa kimatibabu iwapo unauhitaji. Hakika ndiyo sehemu bora ya kwenda kutafuta habari ya hivi karibuni zaidi kuhusu COVID-19 katika nchi yetu.

Kote Ulimwenguni

Sasa unajua unapopaswa kupata taarifa za kuaminika zaidi na taarifa kuhusu janga hili nchini mwetu, lakini je, vipi iwapo ungependa kujua zaidi kuhusu yanayotokea katika sehemu zingine ulimwenguni? Mojawapo ya sehemu bora ya kutembelea ni wasifu wa mtandao wa kijamii au tovuti ya shirika linaloaminika la kimataifa kama vile Shirika la Afya Duniani (WHO). WHO inajishughulisha katika kutafuta habari kutoka kwa madaktari, wanasayansi, na watafiti bora ulimwenguni na ni chanzo kikuu cha sio tu habari kuhusu COVID-19 lakini pia aina mbalimbali za habari ya kiafya! Nchini Kenya unaweza kupata taarifa katika lugha ya Kiingereza- kutoka kwa WHO kwa kuwafuatilia kwenye mtandao kwenye Facebook au kwa kutembelea tovuti yao kwenye.