Yeye ni kama mimi tu

Kutoka kuwa adui hadi rafiki

Yeye ni kama mimi tu

Nilipoanza shule ya upili mara ya kwanza, sikuwa nikihisi nikiwa mzuri sana. Nilifikiria kwamba nilikuwa mwembamba sana, na mrefu sana. Nilipenda kucheza michezo wakati wasichana wengine walipenda kwenye kununua vitu. Gredi zangu zilikuwa sawa lakini sikuwa mtoto mwerevu sana.

Msichana mwingine shuleni, Beth, alikuwa kinyume nami. Hakuonekana akiwa kamili, bali alikuwa na alama nzuri sana. Walimu walimpenda na kila mtu alitaka kuwa rafiki yake. Alikuwa mkarimu kwa kila mtu, ambayo ilimfanya hata asiwe na dosari yoyote.

Lakini sikuwa mzuri kwa Beth. Uwivu ulinifanya niwe mbaya. Singetabasamu au kufanya juhudi zozote za kuwa marafiki tulipokuwa katika darasa moja. Kisiri nilitaka kuwa rafiki yake, hata kama matendo yangu yalionyesha sivyo.

Kisha siku moja, nilipokuwa natembea kuelekea nyumbani kutoka shuleni, nilimwona Beth mbele yangu. Alikuwa anaongea kwenye simu, na ningeweza kusikia akilia polepole.

Alipokata simu, nilijua ninapaswa kufanya kitu. Nilikuwa na wasiwasi, lakini kwa upole nikamgusa begani na nikamuuliza kama ako sawa. Akiwa bado analia, alitabasabu na akasema, 'ndiyo niko sawa, asante'.

Ingekuwa rahisi kwangu kusema ni sawa na niendelee kutembea, lakini badala yake, nikaamua kuwa rafiki na kutembea na yeye

Beth akakubali. Kwa muda tulinyamaza, lakini baadaye tukaanza kuongea. Tuliongea kuhusu mambo ya kawaida, kama vile jinsi mtihani wetu wa sayansi ulivyokuwa na jinsi Bw. Turnbell si mtu mzuri. Tulizungumzia kuhusu mambo mazito pia. Beth alikuwa amekasirika kwa sababu rafiki yake wa kiume alikuwa amemwacha. Alisema kwamba alikuwa 'mnene sana'. Nikafikiria kuwa huo ni wazimu, lakini Beth akaniambia kwamba hajihisi vizuri kuhusu mwili wake.

Jioni hiyo, tulinunua aisikirimu na tukaweza kujuana vyema. Akaniambia kwamba wakati hajihisi ana ujasiri yeye hujiambia maneno mazuri. Sasa wakati wowote mmoja wetu ana huzuni, sisi husaidiana kujengana kwa kusema mambo matatu mazuri.

Kwa mfano, nilimkumusha Beth kwamba alikuwa mkarimu sana, huwa anatabasamu kila wakati na ni mzuri sana katika hesabu kuliko mtu yeyote. Yeye akaniambia kwamba anapenda nywele yangu, uwezo wangu wa kucheza voliboli na yeye hufurahia wakati ninasoma hadithi zangu kwa sauti darasani.

Ni vizuri kujiona kupitia macho ya wengine ili kujikumbusha mambo mazuri unayo.

Sasa, badala ya kuona Beth kama mtu mzuri kuniliko, ninaona tu jinsi sisi wote ni wazuri kwa njia tofauti. Yeye ni mzuri katika hesabu na sayansi, mimi ni mzuri katika kuandika na historia. Hakuna yoyote nzuri au mbaya - ni tofauti tu. Na sisi wote tunapenda voliboli!