Swali – Nipost ama nisipost?

#mambopoapekee

Swali – Nipost ama nisipost?

Utani na mizaha ni jambo la kawaida kati ya marafiki. Na kwenye mitandao ya kijamii tunaweza kuwa wabunifu wa hayo –kwa picha na video za kuchekesha tunazoweza kutumia. Lakini tusipokuwa makini, tunaweza kukasirisha wengine bila kukusudia kwa posti zetu. Jibu swali hili ili kujua ikiwa unastahili kupost kitu fulani au la!


Je, unataka kuposti kitu cha kumtania rafiki yako?

1. Posti yako inahusu udhaifu wowote alionao rafiki yako?

A. Hapana (endelea kwenye swali la 2)
B. Ndiyo. (Wacha kuposti)

Dadangu ishia hapo. Kumtania mtu kuhusu udhaifu wake ni moja ya njia rahisi za kuwaumiza. Inaweza kuchukuliwa kama namna ya kumuonea. Tujiweke kando na mada nyeti kama hizo, sawa?

2. Post yako ina taarifa ama picha ya siri ya rafiki yako?

A. Hapana (endelea kwenye swali la 3)
B. Ndiyo. (Wacha kuposti)

Whoops! Hapana kabisa-hapana maana inaweza kumweka rafiki yako hatarini. Wengine wanaweza kuanza kumkejeli kwenye mtandao. Pia, si poa kushiriki taarifa za siri ambazo sio zako.

3. Hii posti ina matusi au lugha chafu?

A. Hapana (endelea kwenye swali la 4)
B. Ndiyo. (Wacha kuposti)

Hatutakiwi kamwe kutumia lugha chafu kama iliyo kwenye wall yako. Tuweke maeneo yetu ya mtandaoni poa kwa kutumia maneno mazuri.

4. Una uhakika rafiki yako hatakasirika?

A. Ndio (enda kwa Jibu A)
B. Sijui (enda kwa Jibu B)

Jibu A: ENDELEA NA KUPOSTI!

Inaonekana hii posti haina shida yoyote. Endelea na bonyeza tuma!

Jibu B: NGOJA KIDOGO

Ikiwa bado huna uhakika, jiweke katika nafasi ya rafiki yako. Kama mtu mwingine angekufanyia hili, ungejihisi kutukanwa? Hii itakusaidia kuamua vizuri daima.


Natumia mwongozo huu umekusaidika kukabili posti zako. Hata tunapowatania marafiki zetu, tutumie mitandao ya kijamii kwa kuwajibika.