Hauna dada mkubwa? Hamna shida!

Wacha tukusaidie kupata watu unaoweza kuamini!

Hauna dada mkubwa? Hamna shida!

Ni vyema kuwa na mtu wa kuzungumza naye unapokuwa na maswali, wasiwasi au maisha yanapokuwa magumu.

Kuwa na dada mkubwa au jamaa anayeweza kukupa ushauri na mtazamo mpya husaidia sana. Hata kama huna dada mkubwa, mnasihi anaweza pia kukupa usaidizi na mwongozo sawa.

Mnasihi ni nani?

Mnasihi ni mshauri anayeaminika na mwenye kuwajibika unayeweza kuzungumza naye kuhusu lolote. Iwe ni kuhusu shule, marafiki zako, wavulana, familia au ndoto zako. Mnasihi anaweza kukusikiza, akuongoze kufanya uamuzi unaofaa au hata akusaidie kupata nafasi mpya!

Hauhitajiki kumwambia mnasihi wako kila kitu kama hutaki, lakini kuwa na mfumo huo wa usaidizi inamaanisha kuwa wanapatikana ukitaka kuzungumza na mtu au kupata ushauri.

Kuwa na mnasihi sio tu kwa watu wachanga, hata watu wazima wana wanasihi pia! Sio lazima iwe mtaalamu au mtu aliye mbali, mtu mwenye kuwajibika tu karibu nawe unayemwamini na una uhakika anaweza kukupa ushauri mzuri anatosha.

Jaribu kuandika jina la mtu unayefikiri anaweza kuwa mnasihi wako!