Samahani, Shangazi, lakini hizo ni taarifa bandia

Hebu nishiriki nawe ukweli, kwa heshima

Samahani, Shangazi, lakini hizo ni taarifa bandia

Pa!

Whatsapp inatoa arifa. Lazima iwe ni kutoka kwa kikundi cha Whatsapp cha familia.

Shangazi yangu anashiriki mzaha mwingine! Imekuwa ikitokea kwa muda mrefu, na wakati huu ninadhani kuwa ninahitaji kuzungumza na kusema kitu.

Hivi hapa ni vidokezi vyangu kuhusu jinsi ya kukosoa watu wa familia yetu kwa heshima — hasa wale waliotuzidi kwa umri— wanaposhiriki taarifa bandia:

Wasalimie kwa upole

Kabla ya kuwaambia chochote, wasalimie kwa upole. Kila wakati anza kwa "Habari, shangazi yangu mpendwa. Asante kwa habari hii, kwa kweli ninashukuru. Lakini kutokana na ninachosoma, hiyo sio kweli."

Waambie ukweli

Baada ya kuwasalimia, shiriki ukweli. Unaweza kushiriki viungo vya taarifa ya kuaminika inayotokana na taarifa au kutoka kwa tovuti rasmi ya serikali, au unaweza tu kupiga picha ya skrini na uwatumie kwenye kikundi.

Toa sababu zako

Iwapo wamekukasirika, waambie kuwa haukusudii kuwaaibisha, unafikiri tu kuwa ni muhimu kueneza habari sahihi kwa kuwa mzaha unaweza kusababisha taharuki na hali mbaya zaidi.

Sema asante na utoe heshima yako

Baada ya kutoa ukweli na sababu zako zinazokufanya kuupinga mzaha huu, waambie kila wakati asante kwa kukusikiliza na kuwa hii haibadilishi heshima yako kwao.

Vidokezi hivi vimenisaidia kila wakati kukomesha kuenea kwa mzaha katika familia yangu bila kuumiza hisia za yeyote, huku pia nikiueneza ukweli.