Kwaheri vizuizi ....Hujambo nafasi

Huna vizuizi. Huna Vikwazo. Hapa kuna sababu 3 kwa nini...

Kwaheri vizuizi ....Hujambo nafasi

Kuna watu bilioni 7 duniani! Hao ni wengi! Watu bilioni 7 na hakuna mwanadamu mmoja anayefanana na mwingine. Je, unajua hiyo ina maana gani? Humaanisha kwamba hakuna mtu mwingine duniani kama wewe. Sisi sote tuna DNA, macho, masikio na utu tofauti. Hii ina maana kwamba wewe ni wa kipekee. Neno kipekee humaanisha wewe ni tofauti, wa thamani, maalum na mambo hayo yote mazuri.

Maisha yanaweza kuwa magumu wakati mwingine. Wakati watu wanakupuuza ni rahisi kuhisi una kizuizi lakini una mbegu za ukubwa ndani yako. Ukubwa ambao hakuna yeyote anaweza kuuchukua.

Hapa kuna njia 3 kuu za kujikumbusha kuhusu jinsi huna vizuizi:

Kauli ya Asubuhi

Kila asubuhi unapoamka rudia mara 3 kwa sauti na kwa kiburi - "Kwaheri vizuizi...NINA NGUVU...NINA KIPAWA...SINA KIZUIZI.. NINAWEZA KUTIMIZA NDOTO ZANGU." Haijalishi umetoka wapi au yale watu wanasema kukuhusu, Springsters wenzako wanakuamini. Kwa hivyo ni wakati wako wa kujiamini kwamba unaweza kutimiza ndogo zako.

Ona ndoto yako

Baada ya kauli yako ya asubuhi, tafuta mahali patulivu, funga macho yako kwa dakika 10 na uanze kujiona ukiishi ndoto zako zote. Fikiria kuhusu maisha ya baadaye. Ujasiri na kuuongezea.

Jithamini mwenyewe

Chukua muda kufikiria kuhusu kila kitu ulichotimiza hadi sasa na uviandike chini. Je, ulimsaidia mtu kutatua shida, kupata pesa, kupita mitihani yako au pengine hata kuanzisha biashara yako mwenyewe. Mambo haya yote ni mazuri na unapaswa kujivunia kwa kupita changamoto hizo. Ushindi mdogo wa kila siku huifanya iwe rahisi kutimiza ndoto zako kwa sababu hatua baada ya hatua huunda ufanisi mkubwa baadaye.

Kwa hivyo msichana kumbuka, una uwezo wa KUWA MTU YEYOTE unayetaka na KUFANYA CHOCHOTE unachokitaka kwa hivyo endelea kuamini na uvunje mipaka hiyo!