Wasichana, tuna nguvu zaidi tukiwa pamoja!

Tukifanya kazi pamoja tunaweza kuleta mabadiliko.

Wasichana, tuna nguvu zaidi tukiwa pamoja!

Hakuna anayeelewa matatizo ya msichana vizuri zaidi kuliko msichana mwingine. Kwa pamoja tunaweza kuufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri. Hii hapa ni namna unavyoweza kushirikiana na wengine kuleta mabadiliko: 1. Tafuta jamii ya wanawake
Watafute wasichana katika shule au jamii yako ambao wana maslahi sawa na yako na wanataka kutimiza malengo sawa na kutenga muda wa kukutana. Unapenda muziki? Uliza ikiwa kuna wengine ambao wangependa kukutana ili kufanya mazoezi baada ya shule.

2. Anza kidogo, kuwa na lengo mahususi
Orodhesha malengo yako yaeleweke. Unataka nini? Usiogope kuanza kwa suluhisho dogo. Labda wasichana wanaoishi karibu hawawezi kutembea hadi shuleni kwa usalama. Anzisha kikundi ambapo nyote mnatembea kuelekea na kutoka shuleni pamoja.

3. Msikilize mwenzako
Si kila mmoja atayaefikiria kuhusu mambo sawa na wewe na hilo ni sawa. Msingi wa kufanya kazi pamoja kwa ufanisi ni kusikilizana na kuheshimu maoni tofauti.

4. Mjali mwenzako
Hata nini kitokee, mnahitaji kuwa pamoja. Wasichana katika kikundi chako ni dada zako na kulinda uhusiano wa dada ni muhimu. Muwe marafiki, walimu, familia na mfumo wa usaidizi kwa kila mmoja.

5. Shiriki ujuzi wenu
Mojawapo ya njia bora ya kuweza kusaidiana ni kupitia vipaji vyenu. Ikiwa wewe ni hodari wa hisabati, saidia kuwafunza marafiki zako. Rafiki huyo aliye na ujuzi wa ajabu wa kushona atakuwa tayari kukusaidia kwa vazi la tukio maalum ikiwa wewe ni karimu kwa ujuzi wako.

6. Kataa mambo hasi
Kuwa karibu na wasichana ambao hawana chochote kizuri cha kusema hukutamausha. Usiruhusu mambo hasi yaondoshe hisia zako kuhusu mambo. Badala yake kaa na wasichana wanaokutia moyo. Wasichana wanaotumia muda pamoja si lazima iwe tu kuhusu kutembea. Mnaposhiriki ujuzi na kutiana moyo uhusiano wenu unaweza kuwa imara na mtandao wenye thamani unaoweza kuendelea kuwasaidia kutimiza malengo yenu vyema siku za usoni.