Jigundue upya!

Kwa mwaka bora zaidi kwako.

Jigundue upya!

Ni mwaka mpya, wakati bora zaidi wa kutafakari na kuweka malengo ya mwaka ujao Je, kuna jambo umekuwa ukitaka kuanza au unataka kuwa bora?

Iwe unataka kuwa bora katika kutoa hotuba, kupata marafiki wapya, kujaribu mchezo upya au kuanzisha biashara – ndoto zako zote zinawezekana!

Kuanzisha jambo jipya kunaweza kuogofya, lakini hivi hapa baadhi ya vidokezo vya jinsi ya kutimiza ndoto zako.

1. Anza mwanzo

Ndoto yako ni kuwa mwanaanga – hatua yako ya kwanza haitakuwa kwenda angani. Inaweza kuwa kujibu na kuuliza maswali zaidi katika somo la sayansi.

Badiliko kubwa huchukua muda, nenda kwa kasi halisi. Andika hatua tatu ndogo ambazo zitakusaidia kuanza leo. Usisahau kusherehekea mafanikio yako kadiri unavyosonga!

2. Egemea adha

Mahali pako ulipopazoea ni bora. Lakini ni ngumu sana wewe kukua kama haundoki hapo. Kujijaribu kunaweza kuwa hakupendezi – akili yako inaweza kuwa na mawazo kama ‘vipi ikiwa nitafeli’ ‘vipi ikiwa nitaonekana au nitasikika kama mjinga’. Fahamu kwamba hii ni mazoea yako yanazungumza Kwa hiyo wakati mwingine unapata mawazo haya, jiambie ‘asante kwa kujaribu kunilinda – lakini ninaweza’

3. Tafuta usaidizi

Kujifunza kutoka kwa watu wanaokuvutia ni njia bora zaidi ya kujifunza ujuzi mpya. Watu wengi hupenda kuzungumzia mambo wanayoyapenda zaidi na watafurahia kukufunza wanayoyajua. Wafikie kwa kuwaambia jinsi unavyoheshimu wanayoyafanya.

4. Kubali unapojikwaa mara kadhaa

Hata mtu mwenye ujasiri zaidi alihitajika kufanya mazoezi ili kufika alipo sasa. Kila mtu hujikwaa hatua chache katika harakati ya kutimiza ndoto zake.

Labda unajaribu timu mpya ya michezo na usifanikiwe mara ya kwanza – hii ni kawaida na kila unapojikwaa inamaanisha una muda zaidi wa kufanya mazoezi.

Jambo muhimu zaidi unaloweza kufanya ni kutokufa moyo na kujipa muda, utafanikiwa!