Matitizo ya mpenzi wa kiume?

Hii ndio njia ya kuongelea hayo.

Matitizo ya mpenzi wa kiume?

Hebu piga picha ya tukio kama hili:

Umempenda sana mvulana fulani kwa muda sasa. nyote wawili mnaanza kuongea na kisha yule mvulana anakuomba uwe mpenzi wake. Anataka kuyafikisha mambo hayo katika ngazi nyingine.

Unasema ndiyo kufikia sasa mambo yamekuwa yakienda vizuri, lakini ukweli ni kwamba hujui hatua inayofuata inajumuisha nini.

Punde si punde mpenzi wako wa kiume anataka kukutana nawe sirini wakati wote na katika chumba chake wakati wa usiku sana

Nawe hupendezwi na jambo hilo. Huko tayari kulala naye na anaoekana alikuwa akitaka mlale pamoja.

Sasa unahitaji kuongea naye haswa kuhusu jinsi unavyohisi na kisha uamue kama uendelee na uhusiano huo au la.

Hilo linaonekana kuwa azimio kubwa sana. Azimio kubwa sana usiloweza kuliamua peke yako. Sasa utaongea na nani kuhusu jambo hili na utamwendea kwa jinsi gani?

Basi huu hapa ushauri kutoka kwa dada zako wakubwa hapo Springster.

1. Kumchagua mtu afaaye

Unataka kumpata mtu ambaye unaweza kuzungumza naye bila woga wowote na ambaye unaweza kumtegemea akupe majibu ya kweli. Hakikisha yeyote utakayemchagua, ni mtu

  • Mwaminifu
  • Mwenye uzoefu
  • Asiyeweza kukuhukumu

Unahitaji kumchagua mtu ambaye ni mwelewa na ambaye hatakuhukumu. Hutapenda mtu akufanye uone aibu au kuwa na hatia wakati hujafanya kosa lolote.

2. Wakati wa kufunguka

Ikiwa kuna chochote kinachokusumbua, kukizungumzia kutakusaidia kukabiliana na hisia zako. Kufunguka kutakuhitaji uwe jasiri lakini baadaye utahisi nafuu ikiwa utaongea na mtu afaaye. Njia ya kufanyia hivyo ni hii.

  • Usione haya au aibu kuongea kuhusu wavulana. Kumbuka kina mama, shangazi na mahusiano ya muda mrefu zaidi yote yamepitia yale yale unayopitia sasa hivi. Wanaelewa, kwa hiyo tulia na uwe jasiri!
  • Tafuta mahali patulivu na pa kimya ili kusiwe na vizuizi vingi na hakikisha yule unayeongea naye ni mchangamfu na hana usongo.
  • Fanyia mazoezi yale utakayoenda kusema. Ikiwa una wasiwasi huenda ukajawa na woga au kutetemeka. Ni sawa kabisa kufanya mazoezi ya yale utakayosema kwa kujiangalia kwa kioo. Pia kuyaandika chini kutakusaidia.

Maisha yana changamoto nyingi kiasi kwamba huwezi wewe peke yako. Ikiwa utahitaji msaada katika kufanya maamuzi makubwa usiogope kuzungumza na mtu fulani juu ya hayo.