Marafiki wavulana ambo ni marafiki TU

Je, hili linawezekana? Hebu tujue zaidi

Marafiki wavulana ambo ni marafiki TU

Je, ni rahisi kwako kujenga urafiki na wavulana shuleni? Au labda unajaribu kufanya marafiki zaidi na wavulana katika darasa lako na hujui utaanzia wapi?

Kuwa na wavulana ambao ni rafiki tu linaweza kuwa jambo la kufurahisha sana.

Hii hapa ni jinsi ya kudumisha urafiki wako na kuweka marafiki wako wavulana wakiwa marafiki tu!

1. Usiwasikilize watu wengine

Ikiwa muda mwingi uko pamoja na rafiki yako wa dhati mvulana, watu wanaweza kusema mambo mbalimbali. Wanaweza kusema mambo kama vile 'lakini mnaonekana mnafaana sana' au 'itakuwa aibu kutojaribu kuwa pamoja.'

Usiruhusu watu wakushinikize kuingia katika mapenzi kwa sababu una uhusiano.

Weka mazungumzo na rafiki yako yakiwa wazi na uhakikishe kwamba nyote mnajua hali ya uhusiano wenu.

Urafiki mara nyingi husalia kwa muda mrefu ukilinganisha na uhusiano wa kimapenzi, hivyo jivunie kwamba unaupa kipaumbele.

2. Weka mipaka fulani

Kuwa na mvulana kama rafiki kunaweza kukuhitaji uweke mipaka tofauti. Ikiwa yeye ni rafiki yako, basi atafurahia hilo.

Kwanza, kamwe hapaswi kukushinikiza ufanye kitu chochote ambacho hutaki.

Pia, unaweza kutaka kuzungumza naye kuhusu kiasi anachopaswa kukugusa, ikiwa kunacho au mambo fulani ambayo hutaki kushiriki naye kama vile chumba chako cha kulala.

Mwishowe, rafiki yako anapaswa awe mtu unayeweza kumwamini, hivyo hapaswi kuwa mtu ambaye anakimbia na kujulisha marafiki zake kuhusu mazungumzo yenu ya kibinafsi.

3. Furahia mambo yanayofanya urafiki huo kuwa wa kipekee

Kuwa na wavulana kama marafiki kunamaanisha utakuwa unapata maoni kutoka kwa wanaume katika masuala yako. Ni kama kuwa na kaka, nao wanapata dada. Unaweza kujifunza mengi kutokana na kuwa na aina tofauti za watu miongoni mwa marafiki zako.

Unapaswa kujivunia na kuwa na msisimko kwamba marafiki zako wote si wasichana pekee, kwa sababu utakuwa bora zaidi unapokuwa na aina tofauti za watu kama marafiki zako.