Uko tayari kuchumbiwa

Moyo unataka kile ambacho moyo unataka.

Uko tayari kuchumbiwa

Ah, mahaba na mapenzi. Kwa kuwa sasa wewe si mtoto mdogo tena, huenda ukaanza kupatwa na ashiki kwa watu. Hilo ni la kawaida. Au, huenda usiwe na hisia hizo: hilo ni la kawaida pia! Lakini itakuwaje ikiwa HUWEZI. ACHA KUFIKIRIA KUHUSU MTU HUYO?!

Ni sasa? Uko tayari kuanza uhusiano? Kabla ya kuanza kushiriki maisha yako na mtu mwingine, jiulize ikiwa:

Uko tayari?
Kuchumbiwa inamaanisha unashiriki sehemu kubwa — wakati wako, kujitolea kwako, na hisia zako — na mtu mwingine. Huchukua muda kuzoea, na lazima uhakikishe kuwa hauchachawizi kazi yako ya shuleni, familia, au muda wa marafiki. Ni vyema kushiriki wakati wako na mtu, lakini kumbuka usijisahau pia. Penda tu ukiwa tayari, si wakati ambapo uko pweke.

Una uhakika?
Jiulize: kwa nini unafanya hili? Ni kwa sababu marafiki zako wanalifanya? Ikiwa unachumbiwa kwa sababu tu ya kuweza kusema kuwa unachumbiwa, haitakuwa raha kwenu na hisia (zenu nyote wawili!) zinaweza kukwazwa kabisa. Ni sawa kusalia bila mpenzi na kutangamana na kundi lako la wasichana wikendi. Ni wasichana wa kuvutia na wanaoleta raha kukaa nao — ndio kwa maana uko kwenye #squadgoals! Uwe au usiwe na mvuto wa mapenzi, kumbuka kuwa tayari uko sawa, unashangaza na unavutia.

Wewe ni jasiri?
Kuwa na imani na ujiamini, hata unapojua kuwa mambo yatakuwa magumu. Kwa sababu unashiriki maisha yako na mtu mwingine, lazima kufanya maafikiano wakati mwingine. Maafikiano mengine ni sawa, kama vile kutangamana na marafiki zake wikendi hii badala yako. Mengine si sawa. Ikiwa huhisi vizuri, fahamu kuwa si lazima ukubali kila kitu.

Unafahamu?
Wakati mwingine watu huachana, ikiwa unapitia hili, usijali ungali mchanga na huu ndio wakati unaopaswa kujitambua. Hata ingawa kuachana kunaweza kuwa kuchungu, kumbuka kwamba bado una marafiki na familia inayovutia itakayokujali (sababu nyingine ya kutowapuuza unapochumbiwa!). Wanakuunga mkono, msichana!