Je, upo katika kundi baya?

Jifunze kuwa na marafiki wazuri maishani

Je, upo katika kundi baya?

Hujambo dada,

Je, unafikiri upo katika kundi baya kwa sasa, kuwa unatumia muda wako na watu ambao sio marafiki wa kweli?

Kutumia muda wako na kundi baya kunaweza kuathiri vibaya maisha yako. Ni muhimu kujizingira na watu wenye tabia nzuri wanaokuwezesha kujieleza na wanaokutia moyo na kukuunga mkono.

Je, utawezaje kujiondoa kwenye kundi baya na kujiunga na kundi nzuri? Hivi hapa ni vidokezo vya kukusaidia:

  • Tambua jinsi kundi baya linavyokaa. Iwapo unatumia muda wako na watu wanaokucheka, kukudhalilisha na kukufanya usijiamini, basi upo katika kundi baya.

  • Tafuta marafiki ambao wanaweza kukusamehe na kukukubali jinsi ulivyo. Hakuna aliye mkamilifu na wakati mwingine huenda ukamkosea rafiki yako au ukavunja imani yao kwako. Rafiki wa kweli atakusamehe na atataka msonge mbele.

  • Tambua jinsi kundi nzuri linavyokaa. Marafiki wazuri ni watu ambao wakupenda na wanakuamini na wanakuunga mkono kila wakati. Pia wanakusaidia kuepuka kufanya maamuzi yasiyofaa na hawatakushinikiza kufanya mambo usiotaka.

  • Jifunze kutambua watu ambao wana malengo sawa na yako. Chagua marafiki ambao wana ndoto za kusalia shuleni, kupata alama nzuri na kujinyakulia fursa. Wana hatima nzuri sana inayowasubiri - sawa na wewe!

Kupata marafiki wapya sio rahisi, lakini unapokuwa wazi, mwaminifu na mkweli, watu wazuri watakuja kwako.

Urafiki mzuri huja bila kulazimishwa kwa hivyo usiwe na wasiwasi sana kuhusu kile watu wengine wanafikiria kukuhusu. Lenga kuwa mtu mzuri na kundi nzuri bila shaka litakuja kwako!