Macho yote yako KWAKO:

Jinsi ya kung'aa wakati macho yote yako kwako

Macho yote yako KWAKO:

Kuangaziwa wakati mwingine hukufanya uogope. Wakati macho yote yako kwako, ni rahisi kuruhusu hisia hizo za kujishuku kukuingia. Haijalishi ujasiri ambao mtu anaweza kuwa nao, kila mtu ana nyakati za kutojiamini na hofu. Jambo kuu ni kwamba kujiamini ni ujuzi ambao sisi wote tunaweza kujifunza. Vidokezo hivi vinaweza kukusaidia kufungua imani yako kuu iliyo ndani yako na ung'ae zaidi wakati unaangaziwa.

1) Lenga uwezo wako

Hakuna mtu yeyote duniani anayetia fora kwa kila kitu, lakini sisi wote tunatia fora kwa jambo fulani. Tunapaswa kulenga uwezo huu. Kijipenda na kuona thamani yetu si ubinafsi, bali ni jambo muhimu la kujihakikishia zaidi. Je, una sauti nzuri ya kuimba? Panga tamasha ya marafiki! Je, unapenda kuandika? Kwa nini usiande hadithi kwa gazeti la eneo lako? Je, unapenda riadha? Panga mechi kati ya marafiki.

Andika jambo moja unalopenda kujihusu kila siku. Unaweza kuanzisha mfumo wa marafiki na ushiriki mawazo haya mazuri na rafiki. Kulenga mambo hayo yote unayoyapenda kujihusu kutaimarisha kujiamini kwako na kukufanya ung'ae!

2) Jihurumie

Sisi wote hukosea, huchanganya maneno, au kukosea hapa na pale. Hiyo ni sehemu ya kuwa mwanadamu. Jambo muhimu ni kwamba unajihurumia katika nyakati hizi na kujipa motisha. Haya yote na matukio ya kujifunza na yatakufanya uwe na nguvu zaidi. Usijaribu kuzingatia mambo ambayo hayakuenda kulingana na mpango na ulenge mamba yote ambayo yalienda kulingana na mpango!

3) Jifunze kwa wale walio karibu na wewe

Sisi wote hupitia hofu na wasiwasi, haijalishi una umri wa miaka mingapi. Jambo muhimu la kijiamini zaidi ni kujua kwamba ni sawa kuomba msaada na kujivingira mwenyewe na watu wazuri wanaokuinua. Ongea na rafiki unayemwamini wakati una wasiwasi na kama unatoa hotuba au kufanya maonyesho, uliza kama unaweza kufanya mazoezi mbele yao.

4) Sema kwaheri kwa kulinganisha

Daima kutakuwa na watu ambao ni wazuri zaidi kwa mambo mengine kutuliko. Inaweza kuwa gredi nzuri zaidi, au ni wazuri katika michezo, lakini unajua kwamba? Hao si WEWE. Hawana ndoto na mawazo yako yote. Uhalisi wako ni wa kipekee, na ulimwengu unaweza kuwa mahali hapana furaha bila wewe kuwa ndani!

Ni muhimu kugundua vipaji vyako vyote ni thamani ya kipekee ambavyo vinaleta kwa dunia. Wewe ni wa thamani na unafaa kung'aa! Lenga uwezo wako wote kwa sababu kujiamini kutakufanya ung'ae hata zaidi! Kama nyota, kwa kuwa wewe ni nyota.