Njia 5 za kuomba msaada wakati unauhitaji

Jinsi ya kuchukua hatua

Njia 5 za kuomba msaada wakati unauhitaji

Wakati mwingine maisha yanaweza kuhisi mazito kwa sababu ya majukumu na ndoto zako zote. Pengine unajiandaa kwa mitihani au jaribio kubwa; au unataka kuhifadhi pesa zako za mfukoni lakini hujui utawezaje; pengi una ndoto ya kazi fulani lakini hujui jinsi ya kuipata.

Kuomba ushauri kutoka kwa wazazi au mhudumu wako kunaweza kukusaidia kukuweka katika njia nzuri. Ikiwa una matatizo ya kuanzisha mazungumzo, fuata vidokezo hivi vitano...

  1. Vaa viatu vya watu wako wazima. Kwa kufanya hivi, tuna maana kwamba unahitaji kujaribu na kuona hali yako kutoka kwa mtazamo wao. Wanaweza kukupa ushauri ambao hutaki kusikia au ambao humaanisha kazi ngumu kutoka upande wako. Lakini hao ni watu wazima wanaofahamu zaidi kuhusu maisha na panda-shuka zake.

  2. Tafuta muda mzuri, tulivu wa kuzungumza. Ikiwa una uhusiano mzuri, itakuwa rahisi kwako kuwaomba kama unaweza kupata dakika tano za muda wao. Lakini ikiwa hamna uhusiano wa karibu, jaribu kuunda mawasiliano bora nao kwa kusaidia nyumbani au na kazi zao, na kwa kuunda nafasi ambazo mnaweza kuongea.

  3. Ongea kwa uwazi na kwa ujasiri. Andika vizuri unachotafutia ushauri na ujifunze kuisema kwa sauti. Ukionekana kama mtu anayejiamini na unajua unachotaka kusema wataelewa kwamba huna mchezo kuihusu na watajaribu kukusaidia zaidi.

  4. Jiandae. Ukijua aina ya maswali wanayoweza kukuuliza, basi unaweza kuandaa majibu yako vizuri na kuwasaidia kuona mtazamo wako. Maandalizi humaanisha mambo yanaweza kuwa rahisi, lakini kumbuka kusikiliza mawazo yao pia.

  5. Kuwa na Mpango B. Unapoenda kuwaona, wakionekana kutokukubaliana na wewe, usijibishane. Badala yake pumua ndani kiasi na uwe mtulivu. Waruhusu waseme wanachosema, waeleze kwamba unaelewa jinsi wanavyohisi (pengine hawakubaliani na unachotaka kutumia pesa zako za mfukoni nacho, au hawapendi kazi unayotaka) na ungependa kuwa na nafasi ya kujielezea. Jaribu kuafikiana kwa njia ambayo itawafurahisha nyinyi wote. Ikiwa huna muda, hairisha mazungumzo hadi wakati mwingine.

Kuzungumza na watu wazima katika maisha yako huenda ikaonekana wakati mwingine kuwa changamoto, lakini vidokezo hivi vitaifanya iwe rahisi kwako.