Mambo 5 unayoweza kuyashinda kwa msaada kutoka kwa marafiki zako

Hivi ndivyo urafiki wa dhati unavyoweza kuboresha maisha yako.

Mambo 5 unayoweza kuyashinda kwa msaada kutoka kwa marafiki zako

Marafiki wazuri wanaokuunga mkono ni wale wanaotuhimiza kufanya kazi kwa bidii, wanaotukumbatia na kutoa ushauri wakati tunahisi vibaya na kwa ujumla hufanya maisha yetu kuwa bora zaidi.

Hapa kuna hali 5 ambazo unaweza kuzishinda kwa urahisi ukiwa na rafiki mzuri kando yako.

1. Kuachana na mpenzi wako

Kuachana na mpenzi wako huwa wakati mgumu na unaochanganya kwa wengi wetu. Lakini kuwa na marafiki unaowaamini wa kuwategemea huifanya iwe rahisi kupitia maumivu haya ya moyo.

Kuongea na mtu au wasichana wako marafiki kuhusu maumivu unayohisi kunaweza kukupa starehe au kukuchangamsha. Kubangaiza na marafiki zako kunaweza pia kuwa njia nzuri ya kutoa mawazo kuhusu mpenzi uliyempoteza.

2.Ugumu na kazi ya shule

Kwanini usumbuke na kazi ya shule wakati una marafiki?

Kwa hivyo wakati mwingine una matatizo ya kutatua hesabu au kuandika kitabu hicho katika somo la Kiingereza, omba msaada kutoka kwa marafiki zako ambao wanafahamu vyema zaidi masomo hayo kukuliko.

3. Udhalimu

Wakati mwingine mdhalimu atamnyanyasa mtu ambaye anaonekana ako peke yake na hana mtu wa kumtetea.

Lakini wakati una marafiki wanaokuunga mkono ambao unaweza kuwa nao wakati wa chakula cha mchana au kutembea nao baada ya shule, wanakuwa kinga ya ulinzi dhidi ya udhalimu.

Ikiwa tayari unadhulumiwa usiifikirie kama jambo la aibu au la kudhalilisha. Shida ni anayekudhalimu wala si wewe, kwa hivyo ongea na marafiki wako wa karibu na kwa pamoja mnaweza kupata njia za kuripoti udhalimu huo kwa wazazi au shule yako.

4. Matatizo nyumbani

Kuzungumzia kuhusu matatizo unayo nyumbani kwa rafiki wa kweli kunaweza kukupa faraja na matumaini. Kubangaiza na rafiki yako kunaweza pia kuwa njia nzuri ya kusahau matatizo nyumbani ambayo huwezi kuyadhibiti.

Kuchukua muda na kumwelezea rafiki unayemwamini ni njia hakika ya kuimarisha urafiki na kutengeneza urafiki wa maisha.

5. Mashaka uliyo nayo

Pengine unafikiria wewe si mwerevu vya kutosha, au kwamba wewe ni mkubwa sana au mdogo sana - kuwa na marafiki wazuri kunaweza kusaidia kuongezea kujiamini. Marafiki wa kweli ukuhimiza kuona urembo wako wa ndani badala ya kulenga dosari zako.

Kumbuka, rafiki wa kweli yuko hapo kuboresha maisha yako kwa kukuunga mkono, kukujali na kuwa mwaminifu.