Hatua 5 za kutumia kujieleza

Ni rahisi mno

Hatua 5 za kutumia kujieleza

Unakumbuka kuna wakati ulikuwa unahisi ni kama hakuna mtu anakusikiliza?

Pengine ulikuwa na rafiki alikuwa akipinga vile utafanya baada ya kumaliza college. Au pengine wazazi walitakata uwe daktari na sio meneja. Maamuzi haya ni ya muhimu sana na inaweza kufanya uhisi kukerwa na kuonewa. Ama sivyo?

NI muhimu kujieleza na kuhakikisha wengine wanakusikiliza. Labda hujui namna ya kufanya hivi.

Hapa kuna dokezo 5 za kukusaidia!

  1. Amini vile unahisi ndani yako – kama kuna mtu amesema ama kufanya jambo na unahisi sio poa, kuna uwezekano hakiko sawa. Amini kwamba unaujua uonevu wa aina yoyote pale unapouona.
  2. Jiamini lakini pia heshimu wengine – Unapojieleza, ongea polepole na kwa utulivu. Unaweza ondoka kidogo unapohisi hasira ikipanda. Hii itakusaidia utulie na upate jambo la kusema.
  3. Kumbuka kumsikiliza mnayeongea naye – Unaweza kuwa na mtu ambaye hakubaliani nawe, lakini pia yeye anastahili kusikilizwa. Ukifanyi hili utaanza kuelewa kuwa watu ni tofauti na wao hufikiri kwa njia tofauti. Unaweza kosa kukubaliana ni college ipi au ni kampuni gani unaweza kufanya kazi, na hilo ni jambo la kawaida.
  4. Hakikisha unashiriki kwenye mazungumzo kutokana na vile wewe unaona – Tumia “mimi” unapoanza kuongea. Na kusema jambo kama “Mimi naona si vizuri kunikatisha nikiongea” hio ni sawa kuliko kusema “Una tatizo gani? Usinikatishe nikiongea”. Kumbuka watu hujibu vizuri zaidi wanapohisi hawaongelewi wao.
  5. Sema kuhusu mabadiliko unayotaka kuona – Eleza haya kwa utulivu. Kwa mfano, pengine ungetaka wazazi wakubaliane na chaguo lako la college. Waeleze kwa njia nzuri na ya heshima.