Njia 4 za kupata unachokitaka

Jinsi unavyoweza kuongea na wazazi wako na kusikiika!

Njia 4 za kupata unachokitaka

Sote tulikuwa hapo - wakati unataka wazazi wako kukuunga mkono kwa jambo ambalo hujui jinsi ya kulizungumzia. Inaweza kutisha sana!

Lakini hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.... kwa kweli wazazi wanaweza kuwa wasaidizi wazuri wa kukuwezesha kutimiza ndoto zako. Unapaswa tu kujia jinsi ya kufanya hivyo kwa njia nzuri!

Ikiwa unahisi salama na vizuri kujaribu - hapa kuna baadhi ya vidokezo vya kukusaidia kupata usaidizi unaohitaji kutoka kwa watu wanaokujali!

1. Zungumza nao kwa njia ya shukrani

Ni muhimu kujua wakati unaomba kitu. Itaonyesha kwamba unashukuru na unafuraha kwa yale yote waliokufanyia.

Kwa mfano, jaribu kusema "Mama na Baba, ninajua mnashughuli nyingi lakini mkipata nafasi, tafadhali nisaidie na kazi yangu ya nyumbani".

Kuwa na heshimu na kujali kunaweza kusaidia sana katika kuwafanya waseme ndio.

2.Fanya utafiti wako

Mojawapo ya njia rahisi za kuwasaidia wazazi wako kuelewa kwa nini unahitaji usaidizi wa ziada ni kutumia maelezo. Wakati unatumia maelezo ili kuunga mkono maoni yako, kumbuka:

  • kuandika maoni yako
  • kuongea kwa uwazi ili kuhakikishwa unaeleweka
  • kutoa mifano ya kuunga mkono unachoomba
  • kuwasikiliza wazazi wako, huenda wakawa na maoni au maswali pia kwa hivyo jipeeni nafasi na muda wa kuzungumza waziwazi.

Kwa mfano, ikiwa unatafuta kuanzisha biashara ndogo, ongea na wazazi kuhusu ni kwanini unafikiria ni wazo nzuri na uonyeshe kwamba uko huru kupokea maoni kutoka kwao.

3.Kuwa mwepesi na wazi

Iwapo utapata mazungumzo hayaendi unavyotaka, ni muhimu kuwa mtulivu. Sio kila wakati utapata ndiyo - kwa hivyo kumbuka kuwa mtulivu na mvumilivu. Iwapo wazazi wako watasema hapana, kubali maoni yao na uulize maswali ili uweze kuelewa vyema.

Watashukuru kwamba unasikiliza maoni yao na hukupatia nafasi ya kufikiria kuhusu njia tofauti ambazo unaweza kufafanua unachohitaji.

4.Wahusishe katika kila hatua

Unaweza kupendekeza kwamba utawafahamisha kuhusu maendeleo yako na chochote unachoomba msaada.

Kwa njia hii, wataona kwamba unataka kuwajumuisha katika uamuzi wako. Mwishowe, hii ni njia nzuri ya kuunda imani na wale ambao wanakujali na inaweza kukuza mahusiano zaidi ya kusaidiana baadaye.