Njia 3 za kuwa rafiki yako mwenyewe wa dhati

Sikiliza moyo wako na ujiheshimu.

Njia 3 za kuwa rafiki yako mwenyewe wa dhati

Je, kuna wakati unahisi ni kama kuna watu wawili kichwani mwako? Je, kuna wakati unahisi ni kama wanabishana au hawapendani?

Tunaposaidia utu wetu kufanya kazi kwa pamoja, inaweza kutusaidia kuhisi wenye furaha na kuwa na ujasiri zaidi.

Hapa kuna jia tatu za kujaribu:

Tumia heshima.

Ukiwa wewe hukasirikia unapohisi umekosa, hauko peke yako. Lakini umewahi kugundua jinsi tunavyoweza kujizungumzia ndani ya vichwa vyetu kwa njia ambayo hatuwezi kumzungumzia mtu mwingine yeyote?

Kuwa mkali kwako kunaweza kukufanya uhisi uko chini sana. Ungejibishana na mtu anayekuita majina au kusema wewe ni mjinga, sivyo? Kwa hivyo fanya hivyo wakati unajipata unafikiria mambo hayo kujihusu pia.

Ukijipata unafikiria kuhusu kitu ulichokifanya kibaya, fanya unavyoweza kumfanyia rafiki na ubadilishe mazungumzo kwa mambo yaliyofanyika vizuri. Jisamehe, tambua unachoweza kujifunza kutokana na kilichofanyika, na uhisi vizuri kwamba unakua.

Sikiliza.

Huenda umesikia kwamba kujiongelesha ni ishara ya wazimu. Lakini inaonekana kwamba ni jambo zuri sana. Husaidia kupanga mawazo yetu, kupanga mapema na kujidhibiti.

Kwa hivyo jaribu kusikiliza sauti yako ya ndani na kuzungumza na yeye! Unapamka asubuhi, au kwenda kitandani usiku, sikiliza mawazo yako. Iwapo una hofu inayokusumbua usiitupilie mbali. Sisi sote tuna hofu. Ikiwa rafiki angetukujia akiwa na wasiwasi tunaweza kuuliza: ni kwanini una hofu, unaogopa nini kitafanyika? Kuna hatari yoyote ya kweli? Ikiwa kuna hatari ya kweli tutasema jiamini. Kama sivyo, tutasema kuwa mjasiri na ushinde hofu yako. Tunapaswa kuwa wakarimu kwetu pia kama tunavyowafanyia marafiki zetu. Ikiwa tunaamini wana uwezo wa kushinda hofu yao, kwa nini tusiweze kushughulikia yetu wenyewe?

Tumia ushauri wako mwenyewe

Fikiria kuhusu ushauri unaoweza kumpa mtu. Uandike chini, subiri dakika chache, kisha usome. Kwa kweli unaweza kusema unafuata ushauri huo wewe mwenyewe?

Kwa kawaida uhisi rahisi zaidi kutoa ushauri badala ya kuutumia. Na wakati tunahisi tunahitaji ushauri mzuri sisi wenyewe, mara kwa mara sisi uhimizwa na yale watu wengine wanafanya kuliko wanachosema.

Jaribu kuishi kulingana na ushauri wako mwenyewe na utawahimiza wengine zaidi ya maneno yako ya busara. Ni vizuri kuwahimiza wengine, kwa kuwa hutufanya tuwe na furaha zaidi na kuweza kujiamini zaidi.