Njia 3 ambazo marafiki wema wanaweza kufanya uwe na furaha zaidi

Usikabiliane na matatizo peke yako, wategemee marafiki zako.

Njia 3 ambazo marafiki wema wanaweza kufanya uwe na furaha zaidi

Kuwa na marafiki ambao tunaweza kuwategemea hufanya maisha yetu kuwa bora zaidi.

Ikiwa umekuwa ukipitia tatizo sugu maishani mwako lakini hujakuwa na uhakika kama unaweza kuwategemea marafiki zako, endelea kusoma ili ufahamu ni kwanini unapaswa...

1. Msaada wa kukimbilia au kutegemea

Ni vizuri kuwa na rafiki unayeweza kumkimbilia na kujifungua kwake wakati unahisi vibaya. Kujifungua kwa rafiki unayemwamini ni bora zaidi kuliko kuwa kimya kuhusu tatizo lako. Husaidia kuondoa dhiki na kuna uwezekano kwamba utajihisi vyema.

Na unaweza kufanya hivyo pia kwa marafiki zako. Ukigundua kwamba hawako sawa, waulize kama wanataka kuzungumzia matatizo hayo. Unachopaswa kufanya ni kuwasikiliza na kuwakumbatia kwa sababu wakati mwingine hiyo ndiyo unahitaji.

2. Wanaweza kukupa mtazamo mwingine wa kuangalia mambo

Kujifungua kwa rafiki yako kuhusu tatizo ambalo unapitia hukupa nafasi ya kuchunguza njia tofauti za kuitatua.

Rafiki yako anaweza kukupatia ushauri ambao hukuwezesha kuona tatizo lako kutoka kwa mtazamo tofauti, ambao hukufanya uweze kulitatua zaidi!

3. Hukufanya utabasamu zaidi

Marafiki wanaweza kutuburudisha sana kwa kufanya mambo rahisi kama kucheza nje, kutembea bustani au kusikiliza muziki pamoja. Wakati unafurahia na marafiki hutakuwa na wakati wa kufikiria kuhusu mambo yote ambayo yanakufanya ujihisi vibaya.

Hiyo ni kweli pia kwa marafiki zako. Ukigundua kwamba rafiki yako anahisi vibaya, unaweza kumwalika kwa siku ya kuwa na burudani. Hii itasaidia kutuliza akili yake na kumfanya aweze kuhisi vyema zaidi.

Kwa hivyo chochote kila ambacho unapitia kumbuka kwamba hauko peke yako na unaweza kuwategemea marafiki zako ili kupata msaada. Na iwapo marafiki zako wanahisi vibaya, fanya kitu ili ujaribu kuwafanya wahisi vizuri. Kwa sababu hiyo ndio kazi ya marafiki.