Mambo 10 maboyz hupenda…

Na wadada wanafaa kuyapenda pia

Mambo 10 maboyz hupenda…

Umewahi jiuliza ni nini maboyz wengi hupenda kuhusu wadada? Utashangaa, lakini majibu haya ni muhimu kwa wadada pia. Hivyo soma zaidi na utaelewa mambo unafaa kujifanyia…si kufanyia maboyz!

1). Maboyz hupenda wasichana wanaojiamini... lakini pia – mtu hujiskia poa akijiamini na wadada hupenda hivo pia. Hivyo kuwa jasiri kwa manufaa yako mwenyewe. Sio kwa ajili ya maboyz – kuwaWEWE

2). Maboyz hupenda wadada ambao wanajua kuongea na kutoa maoni yao kuhusu mambo…lakini usiwaongelee maboyz tu. Sauti za wadada zinafaa kusikilizwa kama watu wengine. Hivo toa maoni na yasimamie.

Mambo 10 maboyz hupenda…

3). Maboyz hupenda wadada ambao wanaweza kujiamulia wenyewe... na mtu husikia poa sana kama anaweza kujiamulia. Sisi wadada tunapaswa tujisimamie haijalishi wengine wanasema aua wanafikiria nini. Maisha ni yako! #powerkwawanawake

4). Maboyz hupenda wadada wajanja... lakini nani hamkubali mjanga? Ni poa kwenda shule na kupenda elimu yako…si ati ndicho maboyz wanapenda, lakini juu itakusaidia kufikia pale unataka kuwa! Na hicho ndicho cha muhimu!

Mambo 10 maboyz hupenda…

5). Maboyz hupenda wadada ambao hutia wengine moyo... na wadada huwa wanapenda kutia moyo wadada wengine. Kusaidia wengine na kujitoa kwa ajili ya marafiki zako ni kitu poa sana!

6). Maboyz hupenda wadada ambao ni wastahimilivu... na wadada hupenda kuwa wastahimilivu pia. Inabidi uamini unaweza kuvunja vizuizi.#hakunamipaka

Mambo 10 maboyz hupenda…

7). Maboyz hupenda wadada wanaweza shirikiana na wengine... na wadada hupenda ivo pia, sababu kushirikiana ni kitu poa kwa kila mtu! Ushirikiano hufanya kufikia ndoto. Mambo makubwa yanaweza tokea ikiwa maboys na wadada wanaweza kuamua pamoja. Basi lifanyie kazi.

8). Maboyz hupenda wadada walio na msukumo wa kufikia ndoto zao... na wadada hupenda ivo pia. Hivo usiogope kushindwa, jiamini na pigania ndoto zako!

Mambo 10 maboyz hupenda…

9). Maboyz hupenda wadada ambao ni positive... na kukuwa positive hutusaidia kuwa na nguvu na maendeleo maisha. Mambo magumu yanaweza kutokea maishani, lakini usiangalie ugumu. Usibaki tu katika shida lakini tafuta suluhisho.

10). Maboyz hupenda wadada ambao *wanaojipenda… hapa Springsters tunapenda kuonyeshana upendo. Jifunze kuona uzuri ndani yako, sababu maisha yako yana kusudi!

Mambo 10 maboyz hupenda…

Hata kama haya ndio mambo maboyz wanapenda, ni vitu ambavyo unapaswa kuvipenda mwenyewe pia na SIO kwa sababu ya boy.

Hivyo dada – zingatia vile utajijenga na kukua kwa manufaa yako mwenyewe na sio kwa sababu ya jinsi wengine wanafikiri. Utafurahia sana baadaye kwa sababu ya hiki.