Picha nyingi za kujipiga? Ndiyo au La?

Picha nyingi za kujipiga? Ndiyo au La?

Mpendwa Bi. Tech,

Ni jambo baya sana kuchapisha picha nyingi mno mtandaoni? Marafiki zangu wote hufanya hivyo, lakini mwalimu wangu husema inaweza kuvutia wawindaji. Anamaanisha nini haswa? Kuna uwezekano gani wa kuwindwa?

Mwaminifu, Asiye na Uhakika Wa Kumwamini

Mpendwa Asiye na Uhakika,

Hili ni swali zuri sana! Watu wanaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu jambo hili. Teknolojia inapozidi kuboreka, pia inakuwa rahisi zaidi kwa watu kujua vitu vya kila aina kukuhusu kutoka tu kwenye picha moja.

Tuchukulie kuwa unachapisha picha yako ya binafsi na marafiki zako mbele ya shule au nyumba yenu. Yeyote anayeona picha hiyo anaweza kufahamu unaposomea au unapoishi. Kisha anaweza kukupata. Ikiwa hujazima mipangilio yako ya "eneo la kijiografia" (hii ni mipangilio inayoruhusu simu yako kushiriki taarifa kuhusu mahali ulipo na tovuti au huduma nyingine), pia anaweza kufahamu pale picha ilipopigiwa.

Kwa hivyo kuwa salama, huwa vyema kuzima mipangilio ya eneo, kwenye simu yako na mitandao ya jamii kama vile Facebook na Twitter. Tahadhari sana kuhusu aina za picha unazopiga na taarifa unayoweka wazi kujihusu na maeneo yako mtandaoni, kwa sababu hujui anayeweza kuwa akikutazama!

Huenda ukadhani ninawalinda kupita kiasi. Lakini ninawajali wasichana, na ninawataka muwe salama iwezekanavyo.

Mpendwa, Bi. Tech