Sisi wote tunahitaji Washauri!

Mwongozo wa wasichana wa kumpata mshauri mzuri

Sisi wote tunahitaji Washauri!

Haijalishi kama una umri wa miaka 16 au 66, wakati mwingine unahitaji kuongea na mtu!

Washauri ni watu tunaoweza kuwaamini, na hutupatia mwongozo na usaidizi wakati tunauhitaji zaidi. Maisha yetu yanapokuwa yakibadilika, mara kwa mara tuna maswali na hoja ambazo hatutaki kuwauliza marafiki wa dhati au familia zetu na hiyo ni sawa kabisa.

Washauri huja katika maumbo na vipimo mbalimbali na wanaweza kutupatia ushauri kuhusu kitu chochote kuanzia upendo, kazi ya shule, njia za kikazi na masuala ya mwili. Vidokezo na mbinu hizi zitakusaidia kuwapata.

Kuwachagua

Fikiria kuhusu sifa unazopenda katika watu na unachotaka kujifunza. Je, una ndoto ya kuwa mwanamke mchapa kazi? Basi unaweza kupendezwa na kukutana na mtu wa biashara au mjasiri amali. Je, unahisi una haya na hujiamini? Pengine tafuta mshauri katika ulimwengu wa maonyesho ambaye anaweza kukufunza mambo mawili au matatu kuhusu kujihisi vizuri. Je, una sumbuka na kazi ya shuleni au marafiki? Pengine msichana mkubwa wa shule ndiye mtu anayemhitaji.

Kumbuka, mshauri anaweza kuwa mtu yeyote ambaye unampenda kuanzia nyanja za kitaaluma hadi jirani yako. Ni sawa pia kuwa na zaidi ya mshauri mmoja kwa kuwa watu tofauti wanaweza kukupa dhana tofauti.

Kuwasiliana

Kuwasiliana na watu kunaweza kutisha, lakini kumwomba mtu kukushauri ni pongezi. Watu wengi watafurahia kushiriki hekima yao na wewe! Wafuatilie mtandaoni na uwaandikie barua pepe au barua. Unaweza pia kuongea nao katika hafla, au upange mkutano. Hakikisha unakutana nao katika maeneo ya umma na umwambie mtu unayemwamini ni wapi unakoenda.

Kama hujui jinsi yak upata maelezo ya mtu, uliza mwanafamilia, mwalimu au rafiki akusaidie. Mweleze mshauri uliyemchagua kujihusu na malengo yako na kisha uliza maswali mahsusi. Iwapo mtu hatajibu, usipoteze matumaini kwa kuwa kuna watu wengi wazuri karibu!

Ni wazo nzuri kuandaa baadhi ya maswali ya mkutano wako. Mshauri mzuri hatakuwa na shida kujibu maswali yako na atafanya ujihisi salama. Amini hisia zako unapokutana nao, na kama ujihisi vizuri kuongea kuhusu jambo fulani, sio lazima ulizungumzie.

Kujivunia na kushiriki ufahamu wako pia!

Unaweza pia kujishauri mwenyewe. Washauri wakubwa huwa wanajifunza mambo mapya kila wakati na kuomba ushauri wenyewe. Mawazo na uzoefu wako unaweza kuwasaidia wasichana wengine pia. Sauti yako ni muhimu!

Zaidi ya yote, jivunie. Unafanya vizuri na kufikiria kuhusu kupata mshauri huonyesha tamaa yako ya maisha na mustakabali wako. Endelea hivyo!