Vidokezo vya kufanya wasifukazi wako uvutie!

Umepata kazi unayotaka? Wasifukazi mzuri ni hatua ya kwanza ya kuipata.

Vidokezo vya kufanya wasifukazi wako uvutie!

Kazi ni njia rahisi ya kujitegemea kifedha! Ni bora kuwa na wasifukazi ulioandikwa lakini usiwe na wasiwasi ikiwa huna kompyuta yenye kichapishaji, unaweza kuunda wasifukazi wa kuvutia bila ya kompyuta.

1. Orodhesha kazi ambazo umezifanya
Ikiwa umefanya kitu katika uwanja huo sawa na kazi unayotumia ombi, kiweke cha kwanza. Ni sawa ikiwa huna tajiriba, fikiria wakati ambapo umekuwa na cheo cha jukumu katika jamii au shule yako kama kujitolea au kuwa nahodha wa timu. Pia orodhesha maelezo ya elimu, mafanikio (labda ulikuwa kiranja au ulipokea alama za ubora katika elimu au michezo) na usisahau maelezo yako ya mawasiliano.

KIDOKEZO: jaribu kutuma ombi la kazi inayolingana na masomo yako au mambo ambayo unayafahamu vyema. Orodhesha sifa ambazo zinafaa zaidi kazi unayotumia ombi kwa mfano, ikiwa wewe ni bora kwa watoto, kupika, kuzungumza Kiingereza au kucharaza maandishi.

2. Ongeza mrejelewa
Huyu ni mtu ambaye mwajiri wako mtarajiwa anaweza kuwasiliana naye kwa pendekezo – anaweza kuwa mwajiri wa awali, mwalimu, kocha au hata rafiki wa familia katika uwanja huo wa kazi unayotumia ombi. Hakikisha kuwa atazungumza mambo mazuri kuhusu utendakazi wako wa elimu au ujuzi wa kazi.

3. Uunde vizuri
Muundo unamaanisha mahali na jinsi maneno yako yalivyopangwa. Koleza vichwa vyako, pigia mistari maelezo muhimu na uunde aya zilizo na mistari inayolingana. Pia, tumia hoja za matobo au pangilia tajiriba, elimu na/au ujuzi wako ili vivutie.

4. Pata nyenzo zinazofaa
Weka kwenye karatasi nyeupe na wino mweusi ili uonekane kitaalamu. Ikiwa unaandika kwa mkono hakikisha kuwa unatumia kalamu inayofanya kazi vizuri na utumie rula kupiga mistari wima – wasifukazi ambao maandishi yamepangiliwa vizuri huvutia sana. Pia mwombe rafiki, mwanafamilia au mwalimu akague hijai au sarufi yako.

5. Uhifadhi
Ikiwa umeucharaza wasifukazi wako, hakikisha kuwa umehifadhi nakala ya kielektroniki. Ikiwa unatumia kompyuta ya watu wengi kama vile shuleni au duka la mtandao, utume mwenyewe kwa njia ya barua pepe. Pia ni jambo zuri kuhifadhi faili ukitumia kadi ya kumbukumbu au kwenye simu yako kama unavyofanya wimbo au picha.

6. Sambaza wasifukazi wako
Sasa kwa kuwa kazi ngumu imekamilika, ni wakati wa kuusambaza nje. Unaweza kuutuma wasifukazi wako kwa njia ya barua pepe au posta ikiwa ni ombi la cheo ambacho umeona kimetangazwa, lakini ikiwezekana nenda maeneo ambayo ungependa kufanya kazi mwenyewe. Ulizia ikiwa wana nafasi na umpe mtu anayefaa wasifukazi wako. Omba kumwona mtu anayeajiri ukiweza.

Sasa kwa kuwa una wsifukazi, nenda upate kazi. Kila la heri!