Nionyeshe pesa

Kujifunza tabia njema za fedha

Nionyeshe pesa

Unajua nilichojifunza kutoka kwa Shangazi yangu Rita? Jinsi ya kukaanga vibanzi vya kuvutia. Aina tamu sana inayonunuliwa.

Lakini nilijifunza kitu kingine kutoka kwake: jinsi ya kupata hela na kuweka akiba.

Kitu cha kwanza alichoniambia kilikuwa hiki: SI rahisi kupata hela. Kwa kweli. Ndio kwa maana kila siku, ninapaswa kuangalia mapato yangu na kuanglia tena kile nilichokifanya ili kupata hii. Jitihada bila mzaha! Na ninapotumia hela, basi zinakwisha kabisa. Jitihada zangu zote zinakwenda!

Hilo ni Funzo Nambari 1.

Funzo Nambari 2: Itafakari kila siku, haswa pale ambapo jitihada zako zote zitakwenda. Shangazi Rita alianza kuuza vibanzi sokoni. Aliweza kupata hela za kutosha za kuwasomesha binamu zangu. Lakini bila shaka, alichoka kila mara na alifahamu kuwa hili lisingekuwa suluhisho la muda mrefu. Kwa hivyo alianza kuweka akiba, hata alipokuwa na hela kidogo. Na hapo! Yeye na Mjomba wangu Rey waliweza kufungua mkahawa baada ya miaka mitatu.

Hili limenipa msukumo! Si matajiri, lakini Shangazi yangu na binamu zangu wanajitahidi sana. Wanajua namna ya kuweka akiba. Wanafikiria kuhusu siku za usoni wakati wote na hawatumii pesa kiholela. Wanajua jinsi ya kupanga bajeti.

Unda Bajeti Yako Binafsi

“Bajeti” linasikika kama neno la kutisha. Laki sivyo. Ni rahisi kabisa. Hebu tuseme unapata pesa kwa kuuza bangili ulizotengeneza. Weka hizo akiba! Na ufikirie kuhusu unachoweza kuzifanyia: kuwasaidia wazazi wako, au kuzitumia kulipia karo ya shule au karo za ndugu zako.

Njia rahisi ya kuanza kuunda bajeti ni kutenga makopo au bahasha tatu tofauti: moja inayoitwa “weka akiba”, nyingine inayoitwa “tumia”, na nyingine inayoitwa “shiriki”. Ile ya “weka akiba” inapaswa kukusaidia kushughulikia kutimiza lengo fulani. Je, ni pesa kiwango fulani? Au kuweka akiba kwa ajili ya simu mpya? Ile ya “tumia” inaweza kuwa ya matumizi yako ya kila siku, kama vile barafu. Ile ya “shiriki” inaweza kuwa ya vitu kama vile kusaidia kwa karo ya kaka yako, au kufadhili kanisa.

Kufanya mambo kama haya kutakusaidia sana kusambaza pesa zako. Kinyume cha watu wengine wanaotumia pesa moja kwa moja, pindi tu wanapozipata. Wananunua nguo au simu mpya ya mkononi. Lakini haya yatakuwa mazoea baada ya muda mrefu: kutumia pesa bila kufikiri badala ya kuweka akiba.

Kwa hivyo nikifikiria kuhusu kutumia pesa, ninafikiria kuhusu Shangazi kwanza. Sitaki kuuza vibanzi maisha yangu yote! Ndio kwa maana ninapata msukumo kutoka kwake na kujaribu kuweka akiba kwa maisha yangu ya baadaye.