Mjamzito na mwenye matumaini

Kuwa na mtoto hakupaswi kukuzuia.

Mjamzito na mwenye matumaini

Hakuna mtu anaweza kusema kwamba kuwa mjamzito sio jambo kubwa. Ni badiliko la maisha. Lakini haimaanishi umebadilika. Kuwa na mtoto inaweza kuwa mwanzo mpya kwako pia.

mwanzo wa kutisha
Angel hakutarajia kuwa mjamzito katika umri wa miaka 15. Mwanzoni alifikiria elimu yake imekwisha. Alihisi nafasi zake za kupata kazi nzuri na maisha mazuri zilikuwa zimeondoka.

Alilala usiku pasipo kupata usingizi-kutembea huku akisinzia katika siku zake. Hakumwambia mtu yeyote kwa sababu hakuweza kusema kwa nguvu - lakini aliandika hisia zake katika kitabu chake cha kumbukumbu.

Kuweka wazi
Haikuwa hadi rafiki yake wa dhati alipomshawishi sana kumshiriki jambo gani baya ndipo mambo yalianza kubadilika. Rafiki yake aliwasiliana na kliniki mara moja, na baadaye akaenda naye kukutana na wataalamu.

Muuguzi hakuchunguza afya yake tu lakini alimwelekeza wapi anaweza kupata msaada.

Alipokuwa anaandika kwenye kitabu chake cha kumbukumbu usiku huo, Angel alipigwa na butwaa jinsi gani ilivyo rahisi kujisikia vizuri kidogo.

Hatua kwa hatua
Angel aliendelea, akitafuta msaada na taarifa zote kadiri aliyoweza. Taratibu, huku akiosoma kuhusu uzazi, au kwa kuwatazama kinamama wakicheza na watoto wao, alianza kuhisi kama kunaweza kuwa na vitu vizuri vya kutarajia katika siku zijazo.

Rejesha
Usiku mmoja, alipomaliza kuandika katika kitabu chake cha kumbukumbu na akafungua kurasa za nyuma, Angel aliamua kufanya jambo jasiri. Alihisi sana kuwashukuru watu waliomsaidia wiki zilizopita, aliamua kushiriki hadithi yake.

Alitumaini ikiwa kuna mtu kama yeye huko nje, ataweza kuwasaidia. Kwa hivyo aliandika kumbukumbu zake na kuchapisha blogu.

Alishangaa jinsi wasichana wengine walivyoanza kuwasiliana naye kwa haraka kusema kuwa walikuwa wanmepitia hali hiyo. Watu walimshukuru kwa kushiriki hadithi yake - alijua alikuwa amefanya kile alichopanga kufanya - saidia.

Kupata tumaini jipya
Angel alipopata mtoto wake, ilikuwa kazi ngumu, lakini kwa sababu aliweza kushiriki kupitia blogu yake hakuhisi kuwa pekee yake. Alihisi vizuri kila siku kuwa mtoto wake alikuwa anakua vizuri.

Aliombwa hata kutembelea kundi la kinamama wenye rika dogo kuzungumzia simulizi yake. Ilikuwa inatisha lakini baadaye akagundua kwamba ilikuwa kitu alichotaka kufanya zaidi.

Alikuwa na wasiwasi kuhusu elimu yake kuwa asingeendelea, lakini Angel aligundua kwamba alikuwa bado anajifunza, kwa njia tofauti, na kuendeleza ujuzi mpya na matamanio mapya njiani.