Kumpata "anayefaa"

Jinsi ya kumpata mshauri wako

Kumpata "anayefaa"

Sasa uko katika umri ambao una maswali mengi sana kuhusu mambo mengi muhimu! Kuanzia mahusiano hadi chaguo kubwa maishani, wakati mwingine unahisi ni kama itakuwa vizuri kama ungekuwa na mtu unayemwamini anayeweza kukushauri ili uweze kutoa maamuzi sahihi.

Mshauri ni mtu unayeweza kuwasiliana naye na ambaye anaweza kukuelekeza na kukuwezesha ufikirie kwa kini, na kukufanya utoe maamuzi yako mwenyewe kuhusu mambo fulani.

Unaweza kumpata mshauri wako kwa kufuata hatua hizi tano ambazo ni rahisi:

Andika unachohitaji

Ukiandika kwenye karatasi unachohitaji hasa kutoka kwa mshauri unachohitaji, msaada au ushauri, aina ya maadili wanayopaswa kuwa nayo na jinsi unavyofikiria uhusiano utakavyokuwa - itakupatia wazo wazi wa kile unachohitaji.

Tengeneza orodha ya washauri watarajiwa

Andika watu wote katika maisha yako ambao wanakuhimiza kufanya kazi kwa bidii, kujiendeleza na ambao wana hekima ya kukupasha mengi. Pengine ni mjomba wako anayeendesha biashara yake mwenyewe iliyonawiri, msichana aliye darasa la juu shuleni ambaye unampenda au mfanyikazi mwenza kazini ambaye anafanikiwa sana.

Fanya utafiti kiasi

Punde tu una wazo wazi la unachotafuta katika mshauri na umetengeneza orodha yako ya watu unaowapenda, ni wakati wa kuanza kufanya utafiti! Fahamu mengi kuhusu kila mtu kwenye orodha yako. Je, wana maadili sawa na wewe? Je, wana wakati na wako tayari kuwa washauri?

Jaribu

Hadi sasa, pengine umefupisha orodha yako kwa watu wachache. Anzisha mazungumzo na watu hawa, iwapo unahisi salama kufanya hivyo. Waeleze malengo na ndoto zako, na unachotafuta ushauri kuhusu. Waulize maswali kuhusu mambo yote yanayokusumbua - shuleni au kazini, mustakabali wako - na uone watakavyosema. Mara moja utagundua ni nani ako tayari kukusaidia na kukupa ushauri na yule ambaye hawezi.

Fanya uamuzi

Kulingana na mazungumzo yako na watu hawa na unavyohisi kuhusu majibu wanayotoa naya wanavyojibeba wakiwa na wewe, ni wakati wa kufanya uamuzi! Kadiria faida na hasara ya kila mmoja, na punde unapopata anayeweza kuwa mshauri wako, kuwa mjasiri na uchukue hatua.

Unapokuwa ukifuata hatua hizi tano za kumtafuta mshauri wako, usipoteze imani. Mtu unayemchagua kuwa mshauri wako atafurahia sana kukusaidia.