Umekata tamaa kuhusu ndoto zako?

Vidokezo hivi vinaweza kusaidia!

Umekata tamaa kuhusu ndoto zako?

Vipi dada! Fikiria kuhusu hili - Unapopanda mbegu katika udongo haiwezi kumea kwa siku moja. Kulingana na kile ulichopanda inaweza kuchukua wiki, miezi au hata miaka kabla ya kuona kitu chochote! Na hata wakati umepanda kitu chochote huwezi kukipanda tu na kukiacha na kuondoka. Lazima ufanye kazi, kumwagilia mbegu maji ili kuhakikisha udongo una virutubisho vya kutosha ili kumea.

Je! Si hii inalingana na ndoto zetu? Ndoto zako ni kama mbegu, lakini badala ya kuzipanda ardhini zimepandwa ndani yako. Sote tuna mbegu za ukuu ndani yetu. Bila kujali wewe ni nani au umetoka wapi kuna ukuu ndani yako.

Unaweza kuwa unawaza - Ninazo ndoto nyingi lakini zitatimia lini?

Kama mbegu udongoni, kuna kipindi cha kusubiri kati ya wakati unapoamua kufuata ndoto zako na wakati unapoanza kuona maendeleo fulani. Kipindi hicho cha kusubiri kinaweza kuwa cha kuchanganya, lakini hapa kuna hatua kadhaa za kukusaidia kufaulu.

1. Kumbatia safari

Kumbuka kwamba maisha ni safari ndefu sio mbio fupi. Ukuu hautafanyika kwa siku moja na wala ndoto zako pia. Mambo mazuri huchukua muda, hivyo kuwa na subira kwa ajili ukuaji wako. Maendeleo ya muda mrefu BADO ni maendeleo.

2. Furahia safari

Unapotumia muda mwingi ukiwaza mambo yote ya kushangaza unayotaka kufikia siku zijazo, maisha ya kila siku yanaweza kukosa ladha. Siri ya kuwa na furaha ni kutumia siku zako kufanya kile unachopenda. Hakikisha unapanga ratiba ya shughuli za kufurahisha kama vile kushiriki na marafiki au kutafuta mapendeleo mapya.

3. Tafakari wakati wa safari

Wakati mbegu yako inamea itapitia misimu tofauti. Kutakuwa na jua lakini pia kutakuwa na siku za mvua. Kutakuwa na siku nzuri, na vilevile siku mbaya wakati unapohisi ni kana kwamba hufanyi maendeleo lakini hilo halifai kukuzuia kufuata ndoto zako. Kuchukua muda wa kupumzika na kutafakari kunaweza kukukumbusha safari uliyotoka na kukupa motisha unaohitaji kuendelea.