Nini kinatendeka katika mwili wangu?

Ubalehe...kila mtu huupitia!

Nini kinatendeka katika mwili wangu?

Pengine umegundua kuwa mwili wako umebadilika hivi karibuni, sehemu zako za mwili zinabadilika na unapatwa na hisia kwa haraka. Hali hii ni kawaida - inaitwa ubalehe.

Ubalehe? Nieleze mengi zaidi…

Kila mtu ni tofauti lakini kitu kimoja ni sawa kwetu - wavulana na wasichana - sote tunapitia ubalehe. Ni kipindi katika maisha yetu ambacho huonyesha unafikia kuwa mtu mzima. Unaweza anza ubalehe kutoka umri wa miaka 7 au 8 na utadumu kwa miaka minne au mitano. Lakini licha ya tofauti za umri unapoanza, mwishowe sote tunaupitia.

Wakati wa mabadiliko fulani

Mambo mengi yataanza kufanyika mwilini mwako. Yafuatayo ndiyo unahitajika kujua...

  • Matiti yako yataanza kumea
  • Utakuwa mrefu
  • Ngozi yako na nywele huenda ikawa na mafuta zaidi
  • Mwili wako utanenepa na kiuno huenda kikapanuka
  • Huenda ukapata chunusi
  • Utamea nywele chini ya makwapa na kando ya uke wako (mavuzi)
  • Utapata hedhi yako.

Yote kuhusu hedhi yako

Unapobalehe, mojawapo wa mabadiliko muhimu katika mwili wa msichana ni wakati unaanza kupata hedhi.

Katika awamu za kwanza za hedhi yako, homoni zako hukuza mayai kwenye ovari zako. Katika awamu inayofuata, ovari zako huachilia mayai haya. Kwa wakati huo huo, homoni zako zinakusaidia kujenga bitana kwenye tumbo lako la uzazi hivi kwamba iwapo mayai yako yatakutana na mbegu za kiume kupitia ngono, itakuwa tayari kwa ujauzito.

Iwapo mayai hayatakutana na mbegu za kiume, bitana hii huachiliwa kupitia kwa uke katika hali ya uoevu ikijumuisha damu (hedhi yako). Ni hivyo tu - hakuna kitu cha kuogopa au cha kuhofia, ni mwili wako wa ajabu unaofanya mambo ya ajabu!

Ubalehe unaweza kutisha, lakini kumbuka sote tunaupitia - kwa hivyo hauko peke yako!