Ndege na nyuki

Usiaibike, hata maua yanahitaji kuzaa!

Ndege na nyuki

Kujamiiana ni mada kubwa sana — kubwa zaidi kwa makala moja pekee — hivyo tunaigawa katika makala mbalimbali.

Tuanzie mwanzo kabisa: ni nini na kwa nini watu hutaka kufanya mapenzi?!

Ni kupitia kujamiiana ndipo binadamu na wanyama wanaweza kuzalisha; na haya yote ni sehemu ya maisha. Waangalie vipepeo. Inaonekana wanafurahia kupuruka karibu na bustani, husaidia kuchavua, kwa kuweka chavuo katika maua, ili kutengeneza maua zaidi duniani. Inashangaza, sivyo?

Tunapokuwa tungali wachanga sana, akili na mili yetu haiko tayari kuzalisha. Lakini utafika wakati ambapo sote tutafika mahali tutakapoanza kukomaa. Huku ndiko unakoita “ubalehe”. Ni wakati huu ambapo tunapitia mabadiliko mengi ya kimwili na homoni. Kwa wasichana, kubalehe kwa kawaida huanzia miaka 10 hadi 14. (Kwa wavulana, huanza baadaye kidogo — kawaida kati ya miaka 12 na 16.)

Kwa wasichana, kubalehe pia humaanisha kuanza kupata hedhi zako. Pindi tu msichana anapopata hedhi, mwili unakuwa tayari kumbeba mtoto. Hata hivyo, ni jambo jingine kuhakikisha kuwa mtu yuko tayari kihisia kwa jukumu la kuwa na mtoto.

Wakati wa kubalehe, watu wengi huanza kuona watu walio karibu nasi kwa njia tofauti. Huenda kukawa na mtu unayempenda sasa hivi; mtu ambaye huwezi kukosa kumfikiria! Je, hali hii inakufanya uhisi kuchanganyikiwa? Ni sawa! Ni kawaida kuwa na ashiki, jambo ambalo ni la kusisimua pia!

Pamoja na mabadiliko mengi yanayotokea katika mwili wako, mawazo na hisia zote ulizo nazo, na hata unapokuwa wakati wa mapenzi, huenda ukawa umechanganyikiwa na kuwa na maswali mengi. Hata kuhusu kujamiiana. Ni muhimu kuwa na taarifa sahihi kutoka kwa mtu unayemwamini, ili kidogokidogo uweze kuridhika kwa ngozi yako. Kuuelewa mwili wako ni mwanzo wa kujielewa na kujipenda!