Je, unapaswa kuifanya hedhi yako kuwa siri?

Sio jambo la kuonea aibu

Je, unapaswa kuifanya hedhi yako kuwa siri?

Kupata hedhi yako kwa mara ya kwanza ni jambo kubwa! Bila shaka utapitia mihemko ya hisia kwa mara moja – mshtuko, furaha, kuchanganyikiwa, aibu na bilashaka utakuwa na maswali mengi.

Usikusanye hisia hizo zote na wasiwasi kwa sababu uko na hofu ya watakayosema watu wengine. Kumbuka, kila msichana atapata hedhi yake – ni jambo la kawaida la kupitia unapobalehe. Jambo muhimu la kukabiliana na hedhi yako ni kuizungumzia!

Jinsi ya kuwaambia marafiki zako

Ikiwa kundi la marafiki zako halizungumzii kwa uwazi kuhusu kupata hedhi na mambo yote yanayohusu hedhi, basi ni wakati wa kubadilisha marafiki. Kama wewe hujifurahisha na wavulana na wasichana, jaribu kuwa na wakati ambao una wasichana pekee karibu nawe na uanzishe mada hii. Anza kwa kusema jambo kama, “Nimepata hedhi yangu mwezi huu, inasisimua sana! Kuna mtu mwingine amepata yake?” Uwazi wako bila shaka utahimiza marafiki zako kuwa wazi na unaweza kupata mshangao kwamba sio wewe wa kwanza katika kundi lenu kuanza hedhi. Jambo zuri kuhusu kuwa wazi ni kwamba mtaweza kusaidiana kwa ushauri na kujbu maswali.

Jinsi ya kuiambia familia yako

Unaweza ishi na mama yako pekee au wazazi wote wawili au baba yako pekee au na shangazi... haijalishi familia unayotoka, ni muhimu kuwafahamisha walio karibu nawe unayoyapitia. Hii itawasaidia kuwa na fursa ya kukuunga mkono na kukusaidia kununua bidhaa utakazohitaji. Pata muda mtulivu nyumbani kuwaambia. Jieleze unavyohisi – woga, furaha, wasiwasi – na uwaulize kama wana ushauri wowote kwako. Hii itawapatia motisha kutaka kukusaidia, pia wataanza kugundua kwamba umeanza kuwa mtu mzima.

Kumbuka, hedhi ni kawaida ya maisha na wasichana wote watapata hedhi zao hivi karibuni au baadaye. Usijaribu kupitia haya pekee yako. Kwa kuzungumza kuhusiana nayo, utatengeneza mtandao wa msaada wa maana sana.