Fahari ya hedhi au hofu ya hedhi?

Hawa dada mapacha walikuwa na mawazo yanayotofautiana juu ya kuanza hedhi zao.

Fahari ya hedhi au hofu ya hedhi?

Wakati Zena alipopata hedhi yake kwa mara ya kwanza alikuwa na msisimko. Alikuwa amesoma mengi kuihusu na hatimaye ilikuwa inatokea kwake. Hakuweza kusubiri kumwambia pacha wake Amina.

“Oh. Mimi pia,” Amina alisema kwa upole wakati Zena alipompata, na tabasamu likaanguka kutoka kwenye uso wa Zena. Hakuweza kuelewa kwa nini Amina hakumwambia.

Zuena alimshawishi dada yake kuketi na kuzungumza pamoja wakinywa chai.

Amina alihofia kuwa tofauti.

Alidhani kila mtu angeweza kuona amebadilika, ilionekana ni kitu kikubwa sana kwake. Zuena alimwambia kuwa siyo hata yeye, pacha wake, aliweza kusema! Kila msichana anapata hedhi yake kwa wakati fulani, alisema – baadhi mapema, baadhi baadaye.

Amina alikiri alikuwa na wasiwasi kwa sababu ya uvujaji na uchafuko.

Zena alisema – Hakika inaweza tokea, lakini hata kama haupati pedi au visodo tunaweza kutumia tishu au taulo, ili mradi tu makini na safi. Huwezi kuwa na aibu kuomba tishu na kupenga kamasi, hivyo usiwe na aibu kwa hili – sisi sote tuna vitu sawa vya mwili!

Amina alikuwa na aibu kuwa kupata hedhi yake kulimaanisha amekuwa ‘mwanamke’ na sio msichana tena.

Huwezi kugeuka kuwa mwanamke kwa usiku mmoja! Alilia Zena. Ni mwanzo tu, alisema. Miili yetu inapata kuwa tayari kwa ajili ya baadaye – baadaye zaidi. Lakini alikubali kuwa alikuwa na hisia sawa, licha ya kuwa na msisimko kuhusu maisha yake ya baadaye ya utu uzima. Dada hao walizungumza kuhusu vitabu na michezo waliyopenda tangu utoto wao na wakakubaliana kuwa wangetumia muda pamoja kujifurahisha na mambo hayo ya kischana kujikumbusha kuwa haikuwalazimu kuyaacha nyuma, bila kujali umri wao.

Hatimaye Amina alikiri aliumia alipoanza kutokwa na damu na hilo lilimuogopesha.

Zena alielezea uchungu mkali alioupata na Amina alifarijika kwamba alikuwa ameshiriki wasiwasi wake. Ilionekana kama hisia yake haikuwa tofauti sana na ya Zena, na kwamba Zena hakuwa na wasiwasi. Waliamua kutafiti pamoja na kuona kama wanaweza kujua zaidi. Waligundua kwamba maumivu ya hedhi yalikuwa ya kawaida. Hata walipata vidokezo kuhusu jinsi ya kuondoa uchungu, kama kula vyakula vilivyo vya afya, kufanya mazoezi rahisi na kutumia chupa ya maji ya moto.