Nilipata aibu kwa sura yangu

Ubalehe ulinipata mapema.

Nilipata aibu kwa sura yangu

Unapokuwa mtoto una hamu sana ya kukua. Nakumbuka daima nikijaribu kukaa na dada yangu mkubwa na marafiki zake. Ningekasirika wakati watu wangeniambia nillikuwa mdogo sana. Sikujisikia mdogo sana – nilijisikia msichana mkubwa.

Nadhani nilianza kuzungumza mapema sana, kwa sababu kukua sio rahisi kama ionekanavyo. Inakuja na awamu hii ya kuvutia katika maisha inayoitwa ubalehe. Ubalehe ni wakati miili yetu inaanza kupitia mabadiliko kama matiti makubwa na makalio, nywele kwenye mikono na miguu. Ni wakati homoni zetu za kukua zinapoanza. Kwa kawaida inaanza karibu na umri wa miaka 8-13, lakini kwangu ilianza mapema.

Niligundua nilikuwa tofauti wakati watoto wote karibu nami walipoanza kutoa maoni juu ya mwili wangu. Walisema mambo mabayai kama, “Una nywele kama mwanaume.” Au “Mbona matiti yako ni makubwa sana – una ujauzito?”

Kuwa wa kwanza kubalehe kulinifanya kujihisi kama mgeni. Sikupendezwa na mambo ambayo watu walikuwa wakisema juu yangu, hivyo nikashiriki na mamangu kwa sababu ninamwamini.

Mamangu alinifariji sana. Aliniambia nipuuze wanyanyasaji wale. Kwa sababu hawakuelewa mbona nilikuwa tofauti, ilikuwa rahisi kuninyanyasa, lakini ningeweza kuwasaidia kwa kuwafunza. Pia alinifunza kuwa ubalehe ni sehemu asili ya kukua na sipaswi kuwa na aibu kuifikia mapema kuliko watu wengi. Ndio inaweza kuwa hali ya aibu lakini kwa ujumla ni wakati wa mabadiliko ya kusisimua na chanya. Hakuna mtu aliye na haki ya kukuchokoza kuhusu mwili wako.

Kuangalia nyuma wakati yote yalitendeka, niligundua kwamba mazungumzo hayo na mamangu ilikuwa wazo bora zaidi. Kuzungumza naye kuhusu mabadiliko niliyokuwa napitia kulinifanya niwe jasiri na nipunguze aibu. Kwa vile nilifika ubalehe mapema nimekuwa na uwezo wa kuwaongoza wasichana wengine kwatika safari yao. Inaonekana kuna upande chanya kwa kila hali hasi.

Ikiwa wewe ni Springster kama mimi, ambaye amefikia kubalehe mapema, hakikisha hujiwekei hisia zako mwenyewe. Tafuta mtu unayemwamini na uzungumze naye kuhusu hilo. Wanaweza kukusaidia kubadilisha mtazamo wako kwa mambo uwe mzuri zaidi. Usipitie haya pekee yako!