Je, mimi ni Bikira?

Nani huamua? Wewe!

Je, mimi ni Bikira?

Je, mimi ni bikira? Ikiwa umeshaanza kujaribu haya mambo au unataka tu kujua, kuna uwezekano umewahi jiuliza swali hili. Lakini usijali - tunayo majibu kwa ajili yako!

Ni wasichana wachache tu ambao wanajua hili, lakini hakuna maana MOJA iliyokubalika ya ubikira. Wow.

Kama hakuna maana nzuri iliyokubalika, basi inamaanisha ubikira humaanisha kitu tofauti kwa kila mtu. Hii inaweza kushangaza lakini ni poa kwa sababu ubikira Unaweza kuwa jinsi yoyote utakavyo wewe. #MwiliWakoChaguoLako

Hakuna mtu anayeweza kujua ikiwa mwanamke ni bikira au la. Hata madaktari. Inawezaje kuwa na maana?. Najua inashangaza sio?

Acha tuendelee kufuatilia. Wengi husema ubikira huondoka ikiwa uume utavunja kizinda (hymen) ndani ya uke. Hii inamaanisha kwamba msichana si bikira tena baada ya ngono na mvulana. Acha tufafanue hili zaidi:

  • Uume ni ogani ya mwanamume
  • Uke ni ogani ya mwanamke
  • Kizinda (hymen) ni ngozi nyembamba sana ndani ya uke ambayo wanawake wengi, lakini si wote, wanazaliwa nayo.
  • Ngono hufanyika pale uume inapoingizwa ndani ya uke wakati wa kufanya mapenzi.

Ni vizuri kujua kwamba kizinda (hymen) kinaweza kuvunjika unapofanya shughuli za kawaida, kama vile kucheza na sio kufanya mapenzi tu. Sasa hebu fikiria wewe unacheza mchezo wa kupigana kisha unavunja kizinda (hymen) chako. Kweli inamaanisha wewe si bikira tena? Inashangaza kidogo, hapana? Basi kuvunja kizinda (hymen) haiwezi kuwa njia tunayotumia kubaini ubikira.

Na je wavulana nao? Kuna njia ya kujua ikiwa wao ni bikira?

Kimya. Anafikiri, fikiri, fikiri. Anashusha mabega…

Kama tu ilivyo kwa wasichana, hakuna njia ya kubainisha ikiwa mvulana ni bikira. Hii ni sababu nyingine ya kutia shaka maana ya ubikira.

Kama ilivyo kwa vitu vingine maishani, “Ubikira” umetumiwa sana na watu ili kuwaelezea na kudhibiti wanawake na wasichana. Hata hivyo, kama kila kitu kuhusiana na ngono, wewe ndiye unayefanya uamuzi. Bikira au si bikira, nani anayejali? Kuna mambo ya muhimu zaidi ya kuwaza katika maisha yako. Kama vile kufikia malengo na ndoto zako.

Oh na TSUSAHAU kamwe…Haijalishi vile wengine wataongea, wewe ni wa thamani na una kusudi na hakuna yeyote anayeweza kuondoa hilo. Pia una nguvu za kufanya uamuzi wa kibinafsi kuhusu ni nani atakuwa mpenzi wako na mtafanya nini na lini.