Hadithi 5 za uongo kuhusu mimba

Ukweli

Hadithi 5 za uongo kuhusu mimba

Huenda umesikia hadithi fulani kuhusu jinsi ya kupata mimba au jinsi ya kuhakikisha hupati mimba…

Kwa kweli, mbinu ya hakika ya kutopata mimba ni kutofanya mapenzi. Kutofanya mapenzi pia kutakuzuia kupata magonjwa ya zinaa.

Watoto hutengenezwa wakati mbegu za kiume (au mvulana) zinapatana na yai la mwanamke (au msichana). Wakati mume na mke wanafanya mapenzi, mbegu za kiume huogelea kutoka kwa mwili wake hadi kwa mwanamke. Wanawake wengi na wasichana wana mahali maalum miilini mwao panapoitwa tumbo la uzazi. Mbegu zile za kiume huogelea hadi pale. Kama kuna yai pale, basi mtoto anaweza kutengenezwa.

Sasa kwa vile unajua masuala ya kimsingi, hapa ni uongo kuhusu mimba ambao hufai kuamini kamwe.

1. Msichana hawezi kupata mimba kama ni mara yake ya kwanza kufanya mapenzi

Mradi msichana ameanza kupata hedhi zake, anaweza kupata mimba. Haijalishi kama ni mara yake ya kwanza au ya hamsini.

2. Msichana hawezi kupata mimba wakati wa hedhi

Mbegu za kiume zinaweza kukaa ndani ya mwili wa msichana hadi siku 5. Msichana akifanya mapenzi mwishoni wa hedhi yake, anaweza kupata mimba.

3. Msichana akioga punde tu baada ya kufanya mapenzi hatapata mimba

Mbegu za kiume huogelea hadi ndani ya mwili wa msichana. Hakuna idadi ya kuoga itakayoweza kuitoa.

4. Msichana akiruka juu baada ya kufanya mapenzi hatapata mimba

Punde mbegu za kiume ziko ndani ya mwili wa msichana, kuruka juu hakutafanya zitoke nje.

5. Wewe ni mchanga sana kupata mimba

Pindi msichana anapoanza hedhi zake, ana uwezo wa kupata mimba. Haijalishi ana umri wa miaka ngapi.

Kama una maswali zaidi au wasiwasi kuhusu kupata mimba, zungumza na mtu kwenye kliniki. Wanaweza kujadiliana nawe kuhusu mbinu mbalimbali za kupanga uzazi.

Uamuzi wa kufanya mapenzi unahitaji kufikiriwa kwa makini. Zuia kushinikizwa au kukimbilia uamuzi utakao jutia.