Una nguvu zaidi ya unavyofikiria...

Jinsi nilivyopata nguvu baada ya kupoteza wazazi wangu

Una nguvu zaidi ya unavyofikiria...

Hujambo Springster!

Nataka kukusimulia hadithi yangu ...

Maisha yalikuwa mazuri, kila kitu kilikuwa sawa hadi wakati kitu kibaya kilifanyika. Nyumba yangu ilishika moto na nikawapoteza wazazi wangu. Ulikuwa wakati wa huzuni sana kwangu kwa sababu nilikuwa tayari nimempoteza nyanya yangu mwaka uliopita. Ghafla nikawa yatima. Nilikasirika na nilichoweza kufikiria ni: kwa nini jambo hili lilinifanyikia?

Kwa wakati huo sikuhisi kuwa na nguvu ya kutosha kujisaidia. Nilichokuwa nikiuliza tu ni, "kwa nini ni mimi, kwa nini ni mimi, kwa nini ni mimi?" Nilipoendelea kujiuliza zaidi "kwa nini ni mimi?" ndivyo niliendelea kuhisi vibaya. Kuwa na mawazo mabaya kulikuwa kunafanya mambo kuwa mabaya zaidi.

Ghafla wazo likanijia . Nyanya yangu alipoaga dunia nilikuwa na huzuni lakini nikaanza kuhisi furaha tena kutokana na msaada niliopata kutoka kwa marafiki zangu. Kwa hivyo kama nilitoboa awali ninaweza kutoboa tena, sivyo? NDIYO, HIYO NI KWELI! Nilianza kuhisi napata nguvu na ujasiri kutokana tu na kuwa na mawazo mazuri akilini mwangu na kuyasema kwa sauti. Nilianza kukumbuka hali zote ngumu nilizopitia awali. Kila wakati nilipoanguka, niliweza kuinuka tena kila mara. Je, ni kwa nini wakati huu iwe tofauti?

Hujui jinsi una nguvu hadi kuwa na nguvu iwe chaguo la pekee ulilonalo . Baada ya mazishi nilienda kuishi na shangazi na mjomba wangu na wamenisaidia sana tangu wakati huo. Walinisaidia kuelewa kwamba mimi kukasirikia ulimwengu ni jambo la kawaida lakini wakati hufika ambapo napaswa kuinuka tena. Na niliweza!

Shangazi yangu alinifunza pia kauli ninayoweza kutumia ili kujipa moyo. Kila siku nilijisemea, "Kama niliweza kuifanya awali, ninaweza kuifanya tena: Nina nguvu. Nimeokoka. Hakuna kinachoweza kunikomesha."

Baada ya miezi michache ya kurudia kauli hii kila siku, nilianza kujihisi vyema na mwenye nguvu. Hiyo ndio siri ya kuendelea; lazima ujiamini na uwe na ujasiri. Kwa hivyo wakati mwingine unajipata katika hali ngumu au unahisi una huzuni sana, haya ndiyo mambo unayopaswa kufanya:

  1. Kumbuka wakati wa zamani ambapo ulifanikiwa. Jipe nafasi kwa sababu kama uliponea awali unaweza kuponea tena.
  2. Jikumbushe baadhi ya maneno ya kukupa motisha na uyakariri wakati unapoanza kujishuku.
  3. Tafuta msaada kutoka kwa familia na marafiki. Watakusaidia kulenga vitu vizuri ulivyonavyo badala ya ulichopoteza. Cha maana zaidi, daima kumbuka kwamba una nguvu zaidi ya vile unavyofikiria. Usiwahi kusahau hilo.