Je, ulifanya nini leo?

Uzalishaji? Yote yanategemeana na mtazamo

Je, ulifanya nini leo?

Nilikuwa nimezoea kuwa na ratiba yenye shughuli nyingi sana shuleni, ⁠— shughuli za nje ya mtaala kama vile michezo na vilabu, kutembea na marafiki zangu...Siku zangu na wiki zilisonga haraka sana!

Zaidi ya mwezi mmoja uliopita, shule yangu ilifungwa kwa sababu ya janga. Bado masomo yanaendelea, lakini ni tofauti kwa kuwa lazima tusomee nyumbani.

Ingawa mimi kwa kawaida huwa na mambo ya kufanya, kama vile kazi ya shuleni au kuwasaidia wazazi wangu, wakati mwingine siku huonekana kuwa ndefu sana na baadhi ya usiku, ninapoenda kulala, huhisi kama ni muda tangu nifanye kitu chochote cha maana.

Ninapoipitia mitandao ya kijamii, inaonekana kama kuna watu wengi wanaouchukua muda huu kujifunza ujuzi mpya, kuanzisha jambo walipendalo, au kujiburudisha wenyewe kwa kujiunga na shughuli maarufu kama vile mashindano ya mapishi au densi.

Hakuna ujuzi mpya au jambo nilipendalo ambalo ningependa kujifunza. Kwa kweli sijihisi kupika au kudensi sasa hivi. ...Siwezi kujizuia kujihisi kujilaumu kidogo. Je mimi ni mzembe? Ni sawa kwangu kuhisi kutofanya… chochote?

Siku nyingine, nilimwambia mama yangu jinsi nilivyokuwa nijihisi. Aliniambia kuwa kila mmoja hukabili hali za kufadhaisha kwa njia tofauti na kuwa ni sawa kabisa kwangu kuhisi nilivyokuwa nijihisi.

Mama yangu alinikumbusha kuwa watu wengi, kote ulimwenguni, wanakumbana na vizuizi vipya kuhusu wanachofanya na wanakoenda kwa sababu ya janga hili— na kuwa wakati mwingine hii huitwa karantini.

Alisema kuwa sababu inayotufanya kukaa nyumbani ni ili sote tuwe na afya, na kuwa bora ninafanya hivyo, tayari nilikuwa nimefaulu na kutimiza yale yote ambayo nilipaswa kuyafanya.

Baada ya kuzungumza na mama yangu, nilihisi vyema zaidi. Wakati mwingine bado kuna sauti ambayo hunisumbua akilini mwangu, ikiniambia kuwa ninapaswa kuwa ninautumia muda wangu kufanya jambo lingine la muhimu zaidi, lakini hii ni hali ya kufadhaisha kwetu sote, na ninapohisi kupungukiwa, kuwa na wasiwasi, au kuzidiwa, huwa ninajiruhusu tu kuhisi hisia hizo kwa kuwa ni za kawaida kabisa na halali.

...Na iwapo kile ambacho hakika ningependa kufanya sasa hivi ni kutofanya chochote? Hivyo ndivyo nitakavyofanya!

Kando na kazi yangu ya shuleni, jambo la pekee ambalo ningependa kulitekeleza kila siku ni kukaa ndani. Ninaweza kufanya hivyo, na pia wewe unaweza. Sote tuko pamoja katika hili!

....Na ni nani anayejua? Huenda wiki ijayo nitapenda changamoto hiyo ya kahawa ya papo hapo. Lakini na iwapo sitapenda? Pia ni sawa!