Hadithi za kweli: Drama ya Sasha ya hedhi

Jinsi kufikiria kwa haraka kuliokoa mambo!

Hadithi za kweli: Drama ya Sasha ya hedhi

Ulikuwa usiku wa mwisho wa tamasha za drama na nilikuwa na furaha sana kwa onyesho la mwisho. Tulikuwa tunaendelea vizuri na nilipenda jukumu langu katika mchezo ule! Nilikuwa ndege aliyekuwa na fitina na mwerevu aliyedanganya mwindaji na kuokoa ufalme wa wanyama. Hata nilipata fursa ya kupaa juu ya watazamaji kwa wakati mmoja, nikitumia kamba yenye nguvu iliyoshikishwa kwenye dari!

Saa moja kabla ya onyesho, nilianza kuumwa na tumbo. “Bahati mbaya kwangu,” nilifikiria. “Lazima nimekula kitu kibaya.” Nilimeza dawa na nikaamua kusahau. Nilikuwa na onyesho la kufanya.

Nusu ya kwanza ya onyesho ilikuwa nzuri sana, lakini nilipokuwa naingia kwenye jukwaa kwa tukio muhimu sana la onyesho - ambapo ninamdanganya mwindaji na kuwaokoa wanyama wote - nilihisi unyevu katikati ya miguu yangu. “Ah, hapana...” Nilifikiria, ghafla nikashtuka. “Nimeanza hedhi zangu.” Niligundua kwamba ilinibidi nifikirie haraka. Nilikuwa nimevaa jezi nyeupe na kila mtu alikuwa ananiangalia... Lakini nilikuwa na mpango!

Badala ya kupaa juu ya mwindaji na kuwaokoa wanyama, niliamua kuruka ndani ya chungu yake na nimfadhaishe.

Hata ingawa hii haikuwa sehemu ya hadithi, nilipigia kelele kwa wasaidizi wangu wa wanyama kutoka kwenye chungu. “Tafadhali nibebe hadi milimani. Lazima tuharibu chungu cha mwindaji kabla hakijatugeuza chajio!”

Marafiki zangu walichanganyikiwa, lakini nilipatana na jicho la rafiki wangu wa dhati Sarah na nikampa jicho la huruma. Aliwaita wasaidizi wa wanyama haraka na wakanitoa jukwaani haraka. Nilipokuwa pale nilimwambia Sarah kwa haraka kilichotendeka. Alinikumbatia na akaniambia nisiwe na hofu hata kidogo kwa sababu hedhi ni jambo la kawaida. Alinipeleka msalani na kuwaambia wengine wafanye densi ya wanyama jukwaani. Alinipakisodo na sketi ya rangi ya waridi nivae juu ya jezi yangu iliyokuwa na doa. Nilibeba mabawa yangu na nikakimbia jukwaani na kujiunga na densi ya mwisho ya kusherehekea.

Asante kwa fikra za haraka na usaidizi wa rafiki wangu wa dhati, niliokolewa kutoka kwa drama ya hedhi yangu na nikatumia ubunifu wangu kuzuia aibu. Ninajivunia fikra zangu za haraka na nina bahati kuwa na rafiki mzuri kama Sarah kunisaidia katika hali ngumu. Hedhi ni kawaida na sio jambo la kuonea aibu!