Wavulana wale kwenye kona

Wakati ujao nitakuwa mjanja zaidi

Wavulana wale kwenye kona

Nilikuwa njiani kuelekea nyumbani baada ya kukamilisha shughuli jioni moja. Hatua chache kutoka nyumbani niliwaona wavulana wakiwa wametulia kwenye kona. Nilijua walikuwa wachokozi. Sikupunguza mwendo. Sikutaka wajue kwamba niliwaogopa. Hakukuwa na muda wa kurudi nyuma.

Kwa hivyo nilivuka barabara ili kuwaepuka. Lakini walikuwa wakinitazama na kunisubiri. Walivuka barabara na kuanza kunifuata. Roho yangu ilikuwa inadunda Niliingiwa na woga. Walianza kunipigia miluzi na kuniita majina. Wakaniambia “ Njoo nasi mrembo, tunaweza kukufanya utabasamu.” Barabarani hakukuwa na watu. Hakukuwa na yeyote karibu ambaye ningemwomba msaada! Niliongeza kasi ya kutembea lakini walinifuata nyuma.

Nilipopiga kona niliona duka moja limefunguliwa. Nilikimbia kasi kadri nilivyoweza na kuingia ndani. Pindi tu nilipoingia kwenye duka nilihisi vyema zaidi. Sikuwa peke yangu na palikuwa na muuzaji pale dukani. “Tafadhali nisaidie,” nikasema. “Kuna wavulana kule nje wanaonifukuza.” Aliangalia nje na kupiga kamsa. Lakini walikuwa tayari wametoroka. Alimpigia kakangu simu akaja kunichukua na mwishowe nikafika nyumbani salama.

Hali ile ilikuwa ya kuhofisha lakini nilijifunza mambo 3 muhimu kutokana nayo:

  1. Usitembee peke yako usiku. Kila mara jaribu utafute rafiki au mtu mkubwa kiumri katika familia yako.

  2. Epuka barabara zenye giza ambazo hazina watu na zimetulia. Kila mara jaribu upitie kuliko na watu wengi ambako hautakuwa umejitenga.

  3. Kuwa mtu anayeelewa teknolojia. Tumia simu yako kupiga au kutuma ujumbe kwa watu iwapo unahisi upo hatarini. Kwenye programu kama vile Whatsapp unaweza kusambaza eneo uliko kwa watu ndio wajue mahali ulipo.

Mwisho, usitilie maanani watu ambao huwajui wakikuongelesha au kukuchokoza barabarani. Iwapo utajipata katika hali sawa na yangu, usiwache woga ukutawale. Fikiri na utende haraka.